washiriki wa kikosi kazi cha
kujadili mapendekezo ya Sheria ya Ndoa ya 1971 ilikuweza kumlinda mtoto,
wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria
prof Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hoyo Bw. Amon Mpanju
mara baada ya kuzungumza nao juu ya utekelezaji wa jukumu lililo mbele
yao
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na
Sheria prof Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hoyo Bw. Amon
Mpanju akizungumza na kikosi kazi maalum kinachofanya kazi ya kujadili
mapendekezo ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuifanyia marekebisho na
iendane na mahitaji ya wakati uliopo
washiriki wa kikosi kazi cha
kujadili mapendekezo ya Sheria ya Ndoa ya 1971 ilikuweza kumlinda mtoto,
wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria prof Sifuni Mchome
alipokuwa akizungumza nao juu ya utekelezaji wa jukumu lililo mbele yao
Picha ya pamoja
……………………………………………………………
Serikali imeanza mjadala na
baadhi ya wadau ili kupata maoni yao juu ya kuifanyia marekebisho Sheria
ya Ndoa ya mwaka 1971 ili kumlinda mtoto.
Akizungumza katika ufunguzi wa
kikao kazi cha kujadili mapendekezo ya kuifanyia marekebisho sheria ya
ndoa ya 1971 jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba
na Sheria Prof Sifuni Mchome amesema serikali imedhamiria kuifanyia
marekebisho sheria hiyo ili iende na wakati na kumlinda mtoto wa kike
nchini.
“Tumeamua kuifanyia marekebisho
sheria hii kutokana na ukweli kwamba jamii na wanaharakati wameizungumza
sana, huku mazingira yakiwa yamebadilika , kuridhia mikataba ya kikanda
na kimataifa ambayo ina lenga kumlinda mtoto na kufanya Utafiti juu ya
mapungufu yaliyomo katika Sheria ya Ndoa kupitia Tume ya Kurekebisha
Sheria. Hili ni suala ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu hadi ikafikia
jamii kukosa imani na Serikali,na kutokana na hali hiyo tumeamua kuanza
kukaa na baadhi ya wadau ili tuweze kupata maoni juu ya kurekebisha
sheria hiyo,” alisema Prof Mchome.
Alisema Serikali imekuwa ikikerwa
na suala hilo na kuchukua hatua madhubuti za Kisera na Kisheria
kumlinda Mtoto hasa wa Kike kwa kuweka makosa ya kujamiiana (statutory
rape) kwa mtoto chini ya mika 18 na kufanya elimu hadi ya Sekondari kuwa
ya lazima na kuweka marufuku ya kumuoa/kumuoza mtoto wa kike ambaye
bado yuko shuleni, iwe ya Msingi au Sekondari ili aweze kumaliza shule
angalau ya Sekondari na kufikia malengo yake ya kimaisha.
“Serikali imechukua hatua
madhubuti za Kisera na Kisheria ili kumlinda Mtoto wa Kike dhidi ya ndoa
za utotoni kwa kuweka makosa ya kujamiiana (statutory rape) kwa mtoto
chini ya mika 18, kKufanya elimu hadi ya Sekondari kuwa ya lazima; na
kuweka marufuku ya kumuoa/kumuoza mtoto wa kike ambaye bado yuko
shuleni, iwe ya Msingi au Sekondari, nia hapaikiwa ni kumlinda mtoto
hususan wa kike ili aweze kumaliza shule angalau Sekondari na kufikia
malengo yake ya kimaisha,” alisema
Alisema Serikali ilichelewa
kuifanyia marekebisho sheria hiyo kutokana na ukweli kuwa suala la ndoa
haligusi sheria pekee, linagusa pia mila, desturi na imani za dini na
kuongeza kuwa kwa hali hiyo, haitakuwa busara kwa serikali ambayo
inaheshimu imani za kidini na inatambua uwepo wa mila na desturi
zinazofuatwa na makabila mbalimbali na kujichukulia jukumu la kuamua
bila ya kupata maoni na ridhaa ya wananchi na kuongeza kuwa sasa
serikali inaona ni wakati muafaka kuingia katika mjadala na wadau ili
kukamilisha hatua zilizoanza kufanyika kupitia Sera na Sheria nyingine.
Wadau kutoka Shirika la Umoja wa
Mataifa linashughulikia Wanawake-UN-Women, Shirika la Umoja wa Mataifa
linashughulikia Watoto- UNICEF, wanasheria kutoka WILDAF, WILAC, TAWLA
na Wizara ya Mambo ya Katiba Sheria na taasisi zake na Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto,
Post a Comment