Waziri
wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Tanzania anasema kuwa nchi yake
imetia sahihi makubaliano na Uswisi ya kusaidia kurudisha pesa ambazo
zimefichwa kiharamu na raia wa Tanzania katika benki za Uswisi.
Augustine
Mahiga alisema kuwa makubaliano hayo yana sehemu tofauti za
ushirikiano zikiwemo za kubadilishana habari kuhusu uhalifu wa
kiuchumi.
Wabunge wa upinzani nchini Tanzania kwa muda mrefu
wamekuwa wakiilaumu serikali kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya
maafisa na wafanyabiashara ambao wanakisiwa kuficha pesa zao nchi za
kigeni.
Rais wa Tanzania John Magufuli amekuwa akipigana na
ufisadi na matumizi mabaya ya pesa za umma tangu aingie madarakani mwaka
uliopita.
Ripoti ya benki kuu ya Uswisi iliyotolewa mwezi Juni
mwaka 2012 pmoja na matokeo ya uchunguzi wa chama cha wanahabari wa
kimataifa iliiyochapishwa mwaka 2015, ilifichua raia wa wafisa nchini
Tanzania wakiwemo matajiri wakubwa na maafisa wa ngazi za juu serikalini
ambao walikuwa wameficha mamilioni ya dola katika benki za Uswisi.BBC SWAHILI
|
Post a Comment