Mkurugenzi
Mtendaji Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida
akitoa neno la ufunguzi katika halfa ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo
ya Afrika 2016.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo
akizungumza kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
katika halfa ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2016.
Mgeni
rasmi katika halfa ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2016,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Sihaba Nkinga akitoa hotuba kwa niaba ya serikali na kueleza
mikakati ambayo wameipanga ili kuweka usawa wa kijinsia kati ya wanawake
na wanaume pamoja na kuwawezesha wanawake ili waweze kushirki katika
shughuli za maendeleo.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria halfa hiyo
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Sihaba Nkinga akikata utepe kuashirikia kuzinduliwa kwa Ripoti ya
Maendeleo ya Afrika 2016.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Sihaba Nkinga akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Utafiti wa Uchumi
na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi Mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (wa tatu
kulia), Mkuu wa Kitengo cha Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Timothy Mgonja na Mwakilishi wa UN Women
wakionyesha kitabu cha Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2016.
Wageni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya halfa ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Afrika 2016.
Na Mwandishi Wetu
Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) likishirkiana na Taasisi ya
Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) limefanya uzinduzi wa Ripoti ya
Maendeleo ya Afrika 2016 ambayo imekuwa na kauli mbiu ya Kuongeza Kasi
ya Kuweka Usawa wa Kijinsia na Kuwawezesha Wanawake.
Akizungumza
kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo
alisema kuwa ripoti hiyo inaonyesha jinsi gani watu wanaoishi Afrika
wanapiga hatua kupata maendeleo lakini wakikabiliwa na changamoto usawa
wa kijinsia na uwezeshaji kwa wanawake.
"Kupitia
ripoti hii UNDP inaonyesha jinsi gani watu wanaoishi Afrika
wanajihusisha na shughuli za maendeleo lakini bado kuna changamoto ya
usawa wa kijinsia, jambo la kijisnia linagusa kila sehemu kuanzia
serikalini, taasisi za kijamii, mashirika binafsi na hata kwenye vyombo
vya habari,
"Kwa
sasa Afrika ndiyo ya mwisho kwa maendeleo ya binadamu kulinganisha na
sehemu zingine duniani na jambo la usawa wa kijinsia linabaki kuwa
muhimu, UNDP itaendelea kushirikiana na serikali kusaidia kupatikana
usawa wa kijinsia na uwezeshaji kwa wanawake ili kumaliza vitendo hivi
ambavyo vinachangia Afrika kuwa nyuma kimaendeleo," alisema Dabo.
Nae
mgeni rasmi katika uzinduzi wa ripoti hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga alisema
serikali inafahamu kuwepo kwa changamoto hiyo na imekuwa ikichukua
hatua mbalimbali ikiwepo kuwapa nafasi za uongozi wanawake.
Alisema
ripoti hiyo itaisaidia Serikali kuweza kuweka mikakati bora na ambayo
itaweza kumaliza tatizo la usawa wa kijinsia ikiwa ni pamoja na
kuangalia kwa jinsi gani watawawezesha wanawake ili waweze kujihusisha
na shughuli za maendeleo ambazo ziwasaidia kukuza kipato chao lakini pia
taifa kwa ujumla.
"Ripoti
hii itasaidia kupata mipango ambayo inaweza kutumiwa kwa ajili ya
changamoto iliyopo ya usawa wa kijinsia, ripoti inaonyesha jinsi gani
wanawake wanaweza kusaidia kuleta maendeleo lakini bado wanakabiliwa na
tatizo la usawa na hivyo kukwamisha ukuaji wa uchumi,
"Naomba
niwahakikishie serikali ya Tanzania itakwenda kuitumia ripoti kuboresha
sera, mipango na vitendo ili kupatikana usawa wa kijinsia na pia
kusaidia kukuza uwezeshaji kwa wanawake wa Tanzania, serikali imekuwa
ikisaidia kuweka usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na hata
makamu wetu wa Rais ni mwanamke na katika hili tutahakikisha wanawake
wanaendelea kupata nafasi na kusaidia kuleta maendeleo," alisema Nkinga.
Kwa
upande wa ESRF kupitia Mkurugenzi Mtendaji, Dk. Tausi Kida alisema
"Tunafahamu kuwa usawa wa kijinsia ni jambo ambalo limekuwa likitafutiwa
ufumbuzi tangu tukipata uhuru na katika hilo (ESRF) tumekuwa tukiunga
mkono jitihada za serikali kwa ajili ya kuweka usawa kwa Watanzania,
tunaamini ripoti itasaidia kuleta maendeleo kwa Tanzania katika mpango
wa maendeleo ulizindiliwa Dodoma"
Post a Comment