Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa(Picha Maktaba) |
Na
JamiiMojaBlog,Mbeya 12
Mkazi wa
Makongolosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Ndugu Amoke Mbilinyi (25)amefariki dunia katika vurugu zilizotokea leo baina ya jeshi la polisi na
wananchi katika Mji Mdogo wa Makongolosi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .
Katika
vurugu hizo pia askari polisi wanne pamoja na raia watatu wamejeruhiwa kufuatia
vurugu hizo ambazo zilidumu kwa zaidi ya masaa8
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Chunya Ndugu Rehema Madusa ambaye pia
ni Mkuu wa Wilaya hiyo amethibitisha kutokea kwa vurugu hizo ambapo amesema merehemu amefariki dunia wakati akikimbizwa
hospital kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kupata majeraha wakati wa
vurugu hizo .
Amesema tukio
hilo limetokea majira ya saa 4 Desemba 18 asubuhi na limesababisha uharibifu wa mali za
jeshi la polisi kwa kuchomwa moto kituo cha Polisi Makongolosi pamoja na
kufanya uhalibufu wamiundombinu ya barabara pamoja na askari na raia kujeruhiwa ambapo majina ya majeruhi hao
wote bado hayajafahamika.
Aidha Madusa
amesema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa wawili wa
mauaji ya mzee mmoja ambaye jina lake halijafahamika ambapo wananchi waliwataka
Polisi kuwaachia huru ili wajichukulie sheria Mkononi.
Amesema Jeshi la Polisi liliendelea kuwashikiria
watuhumiwa hao ndipo wananchi walianza kuwashambulia Polisi kwa mawe sanjali na kufanya uhalibifu mwingine .
Aidha Mkuu
huyo wa Wilaya amefika katika tukio hilo na kuzungumza na wananchi ambapo
aliwataka kuacha tabia ya kujichukulia sheria Mkononi huku uchunguzi zaidi wa
unaendelea kufuatia tukio hilo.
Mwisho.
Post a Comment