Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye
Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameitaka jamii kuzingatia haki na
usawa kwa watu wenye ulemavu nakuondokana na imani potofu za kuona watu
wenye ulemavu hawana uwezo wa kufanya shughuli za maendeleo.
Mhe.
Possi ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipotembelea Vituo na Shule
zinazohudumia watu wenye mahitaji maalum vya Nandanga, Rasi Bula, Shule
ya msingi Nyangao mkoani Lindi pamoja na makazi ya wenye ulemavu na
Ukoma ya Mkaseka, Chuo cha wenye Ulemavu cha Mtapika, shule ya Lulindi
na Masasi mkoani Mtwara.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee
(wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake katika shule ya Masasi yenye
kuhudumia wenye ulemavu Mkoani Mtwara.
Katika
ziara hiyo Mhe.Possi alisisitiza jamii zibadili mitazamo hasi juu ya
masuala ya haki na usawa kwa watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha
katika shughuli zote na kuwapa vipaumbele vya fursa sawa.
“Ninasisitiza
jamii ibadili mitazamo dhaifu juu ya haki na usawa wa kuwashirikisha
watu wenye ulemavu kwani wana uwezo wa uzalishaji endapo tutawapa fursa
sawa kama ilivyokuwa kwa wakina mama walipoachwa nyuma muda mrefu ila
jamii imeona fursa ndani yao, iwe hivyo hivyo kwa watu wenye ulemavu”
alisema.
Aidha Waziri Possi ameweka mkazo juu ya kuwahusisha na kutokuwaona kuwa ni kundi la kuachwa nyuma na kama tegemezi.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akionesha namna ya kutumia Kurunzi ya mwanga wa jua kwa baadhi ya
wazee wenye ukoma wanaoishi katika Kambi ya Mkaseka Wilaya ya Masasi
Mkoani Mtwara na kuwapatia wazee hao kurunzi 20 kwa kila nyumba.
“sheria
zipo wazi kabisa zinazotuelekeza juu ya haki na usawa kwa watu wenye
ulemavu kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya watu wenye Ulemavu namba 9 ya
mwaka 2010 inayoeleza haki za watu wenye Ulemavu kuwahudumia kwa haki
na usawa na kuboresha maeneo muhimu ikiwemo fursa za kielimu, ajira,
kiuchumi na kijamii,” alieleza.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti alikiri
kuyapokea yote aliyoeleza Mhe.Waziri katika ziara yake na kuipongeza
Serikali kwa juhudi za kuisaidia jamii bila kujali hali zao na tofauti
zao.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi (wa kwanza kushoto) akiwa katika ziara ya kuangalia maeneo ya
shule ya Masasi inayohudumia wanafunzi wa mahitaji maalum wakati wa
ziara yake mkoani Mtwara.
“Ninaipongeza
Serikali ya Awamu ya Tano inayowajali wanyonge na kujali haki zao
pamoja na mhe. Waziri kwa kuona umuhimu wa kututembelea wana Ruangwa na
tunaahidi kukuweka katika kumbukumbu zetu maana umewagusa wakazi wa
Mtwara hususani wazee na watu wenye ulemavu.”Alisisitiza Mkuu wa Wilaya
hiyo.
Nae
Afisa Mfawidhi kituo cha Kulelea wazee wenye ukoma cha Mkaseka Bw.
Cleophace Nguli aliiomba Serikali kuendelea kuwakumbuka watu wenye
ulemavu ikiwa ni watu waliosahaurika na kuendelea kupongeza hatua
zilizopo kwa sasa.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akikagua moja ya bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum la Shule
ya Masasi Mkoani Mtwara.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Halima Dendego akimweleza Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi historia fupi
ya mkoa huo wakati wa ziara yake mkoani hapo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi (wa sita kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara mara bada ya
kumaliza ziara yake mkoani hapo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari katika ziara yake
alipotembelea Shule na Makazi ya wazee Wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.
Post a Comment