Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
mc

SERIKALI inatarajia kuanzisha tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs) nchini kuanzia mwaka 2017.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Aidha, Waziri Nape alisema kuwa tayari Serikali imeanza mazungumzo na makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapatikana kwa uwazi.
“Tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi hivyo makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini mashindano hayo yatakayojielekeza kwenye nyanja tofauti” alisema Waziri Nape.
Waziri Nape pia alisema amewataka wamiliki na watendaji wa blogs nchini kushirikiana na Serikali ili kuweza kuijenga nchi.
“Tutumie fursa za kisiasa zilizopo, fursa za teknolojia ili kuhakikisha tiunajenga Tanzania tunayoitaka, ishaurini Serikali kwa kutumia taaluma mliyonayo ili kuweza kuipeleka nchi ya Tanzania tunayoitaka” alifafanua Waziri Nape.



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top