Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
teta

Balozi wa Japani nchini Tanzania Masaharu Yoshinda (kushoto) na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la kimataifa la Japani (JICA) Bw.Toshio Nagase,(kulia) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mh.Dkt.Philipo Mpango (mb) (hayupo pichani) kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Japani katika sekta ya miundo mbinu zikiwemo barabara nchini Tanzania,mazungumzo yaliyofanyika makao makuu ya Wizara jijini Dar es salaam.
teta-1
Ujumbe kutoka Japan ukiongozwa na Balozi wa Japani nchini Tanzania,Masaharu Yoshinda,ukisikilizwa kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango,Mhe.Dkt.Philip Mpango (hayupo pichani) kuhusu azma ya Tanzania kuwa na Bandari itakayohimili ushindani barani Afrika.
teta-2
Maafisakutoka Tanzania walioambatananaWaziriwaFedhanaMipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupopichani), katikakikaonaBaloziwawaJapaniNchini Tanzania, MasaharuYoshindawakinukuuMaelezoyaliyokuwayakitolewa, kuhusuumuhimuwaMiundombinuikiwemobarabaranarelikwamanufaayawatanzania, wakatiwalipokutananakufanyamazungumzoMakaoMakuuyaWizarayaFedhanaMipango, Jijini Dar es salaam.
teta-3
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt.Philipo Mpango (mb),akisisitiza jambo kuhusu kuharakisha maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu itakayokuwa chachu ya kufikia uchumi wa kati na unaotegemea viwanda,wakati Balozi wa Japana na ujumbe wake walipotembelea na kufanya mazungumzo na Waziri huyo katika makao makuu ya Wizata ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
teta-4
Balozi wa Japani nchini Tanzania ,Masaharu Yoshinda (kushoto) akieleza mtazamo wake kuhusu umuhimu wa kufungua mikoa ya kanda ya kati na Magharibi mwa Tanzania kwa miundo mbinu ikiwemo barabara na reli ambayo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt.Philip Mpango (mb)alimweleza Balozi huyo kuwa ina faida kwa maendeleo ya nchi walipokutana na kufanya mazungumzo makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango,jijini Dar es salaam.
teta-5
Waziri wa Fedha na Mipango,Mhe.Philipo Mpango (mb) wa kwanza kulia akisikiliza maelezo toka kwa Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la kimataifa la Japan (JICA) kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa ujenzi wa barabara mkoani Arusha na maeneo mengine nchini kikao hicho kimefanyika Makao Mkauu ya Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.





Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top