Shirika
la Umoja wa Matifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) limefanya uzinduzi wa kozi ya maadili kwa walimu ambao
wanafundisha vyuo vya afya na sayansi kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika ufunguzi wa kozi hiyo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa
UNESCO, Zulmira Rodrigues alisema UNESCO imeandaa kozi hiyo ili
kuwajengea uwezo kuhusu maadili mema ya kazi walimu hao ili hata
wanafunzi wanaowafundisha wawe na maadili mema sasa na hata baada ya
kuhitimu masomo yao.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues akitoa neno la
ufunguzi katika kozi ya siku nne kwwa walimu wa vyuo vya afya wa ndani
na nje ya nchi.
“Kwenu
wanufaika wa kozi hii ambao itafanyika kwa siku nne, ni matumaini yangu
kozi hii ya siku nne itatumika kikamilifu katika maisha yenu ya kila
siku, ikiwa kama ni mkufunzi, mwanafunzi au katika tafiti zenu za
kisayansi, na utakuwa balozi wa UNESCO kwa kusambaza elimu kwa wengine,
“Jambo la muhimu ni kujenga uelewa ili kuhakikisha kama nchi inapambana
na changamoto kubwa za kimaadili ambazo zinaikabili kwa sasa na baadae.
UNESCO itaendelea kushirikiana na Muhimbili na wadau wengine wa ajili ya
kusaidia Tanzania,” alisema Zulmira.
Mkuu
wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues akizungumza na
washiriki wa kozi ya maadili kwa walimu wa vyuo vya afya.
Kwa
upande wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha
Muhimbili, Prof. Ephata Kaaya alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa walimu
hao na kuwahakikishia kuwa kila mshiriki hataondoka bure kwani watapewa
mafunzo na wakufunzi wenye uwezo mkubwa. “Niwahakikishie washiriki wote
wa kozi hii ambao mnatoka ndani na nje ya nchi kuwa mafunzo haya
yatawaongezea uelewa kuhusu maadili mema, hili tatizo sio la Tanzania
pekee hata Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda wote wanakabiliwa na hili
tatizo kama ilivyo kwetu,” alisema Prof. Kaaya.
Makamu
wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, Prof. Ephata
Kaaya akizungumza kuhusu kozi ya maadili kwa walimu wa vyuo vya afya na
kuahidi kuwa mafunzo hayo yatakuwa bora na ambayo yatakuwa msaada mkubwa
kwao.
Aidha Prof. Kaaya aliishukuru UNESCO kwa kutoa mafunzo hayo na kuwaomba kuendeleza ushirikiano uliopo kati yao.
Baadhi ya washiriki wa kozi ya maadili ya siku nne iliyoandaliwa na UNESCO.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
Post a Comment