Hapa
ni katika ukumbi wa mikutano hotel ya Empire mjini Shinyanga ambapo leo
Jumatano Desemba 21,2016 waandishi wa habari mkoani Shinyanga wamepewa
mafunzo kuhusu masuala ya watu wenye ualbino.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha watu wenye Ualbino nchini (TAS) kupitia programu ya Elimu kwa Jamii kuhusu mambo ya Ualbino 'Community Awareness Raising Program' inayofadhiliwa na shirika la Open Society Foundations.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha watu wenye Ualbino nchini (TAS) kupitia programu ya Elimu kwa Jamii kuhusu mambo ya Ualbino 'Community Awareness Raising Program' inayofadhiliwa na shirika la Open Society Foundations.
Aliyesimama
ni katibu wa Chama cha Watu wenye Ualbino mkoa wa Shinyanga Lazaro
Anael akizungumza katika semina hiyo ambapo alisema lengo la semina hiyo
ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ili waweze
kuandika habari sahihi zaidi kuhusu masuala ya watu wenye ualbino.
Katibu wa Chama cha Watu wenye Ualbino mkoa wa Shinyanga Lazaro Anael
akizungumza.Kulia ni Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye
Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner
Mgeni rasmi Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga George Mdoe
aliyemwakilisha kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akifungua semina
hiyo ambapo aliwasisitiza waandishi wa habari kuendelea kushirikiana na
jeshi la polisi katika kutoa taarifa mbalimbali kuhusu masuala
yanayohusu watu wenye ualbino.
Hata hivyo aliitaka jamii kuacha uoga katika kutoa ushahidi katika kesi za watu wanaojihusisha na mauaji ya watu wenye ualbino
Alisema hivi sasa serikali inahitaji watu wenye ualbino wajumuike katika
jamii ndiyo maana baadhi yao wameondolewa katika kambi zao mfano
Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kurudishwa katika jamii yao
ili kuondoa tofauti yao na watu wengine katika jamii
Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania
Josephat Torner akiteta jambo na mwezeshaji katika semina iliyolenga
kuwajengea uelewa zaidi waandishi wa habari kuhusu masuala ya watu wenye
ualbino, bwana Kadama Malunde,ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya
waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu
Semina inaendelea
Bi
Nabaggala Edith ambaye ni Mkurugenzi wa shirika linalojihusisha na
masuala ya watu wenye ualbino nchini Uganda (Albinism Support
Association Uganda ASAU) akifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini Mwezeshaji
katika semina hiyo Kadama Malunde akiwasilisha mada kuhusu mchango wa
vyombo wa habari katika vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ualbino
nchini Tanzania.
Malunde alisema vyombo vya
habari vimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuongeza ufahamu wa jamii
juu ya masuala ya watu wenye ualbino kitaifa na kimataifa,kupunguza
matukio ya ukataji viungo vya watu wenye ualbino na mauaji, kuelezea
juhudi mbalimbali za TAS kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Malunde
alisema ni kupitia vyombo vya habari hata wadau wamefika nchini na
kuchangia kuboresha hali na maisha ya watu wenye ualbino na kufanikisha
kuanzishwa kwa siku ya watu wenye ualbino duniani ambayo hufanyika kila
mwaka tarehe 13 kila mwezi Juni
Hata
hivyo Malunde alisema bado kuna unyanyasaji wa kijinsia ambapo akina
mama waliozaa watoto wenye ualbino wengi wao wamekimbiwa na waume
zao,wameachika,wametelekezewa watoto na pia watoto wenye ualbino nao
wametekelezwa na kwamba bado kuna mkazo hafifu katika sera na sheria
kuhusu masuala ya mauaji ya albino.
Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania
Josephat Torner akizungumza katika semina hiyo ambapo alisema ipo haja
ya kuondoa majina yanayodhalilisha na badala yake itumike "Watu Wenye
Ualbino" na siyo maneno mengine.
Afisa programu kutoka Chama Cha Watu wenye ualbino Tanzania,Severin Edward akifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania
Josephat Torner akisikiliza hoja kutoka kwa mwandishi wa habari gazeti
la Jamboleo Stephen Kidoyayi
Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akielezea jambo
Picha ya pamoja washiriki wa semina hiyo
Picha ya pamoja
Picha zote na Shinyanga Press Club
Post a Comment