Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiweka fedha mara baada ya
kuzindua tawi jipya la benki ya Maendeleo la Kariakoo, jijini Dar es
Salam, nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ibrahim
Mwangalaba akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Amulike Ngeliama
(kulia).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Maendeleo Banki Ibrahim Mwangalaba akiteta jambo na baadhi
ya wateja wa kwanza waliyohudhuria ufunguzi wa tawi jipya la Kariakoo.
Askofu
wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiweka wakfu na kuzindua tawi jipya
la Maendeleo banki, Kariakoo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti
wa Bodi, Amulike Ngeliama, na kushoto ni Mkuu wa Jimbo la Kati Mch.
Frank KImambo
Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa tawi la Kariakoo.
Baadhi
ya Viongozi wa Maendeleo Bank wakiwa katika picha ya pamoja watatu
kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi Nuru Shadrack katika uzinduzi
uliofanyika Kariako na kuzinduliwa na Baba Askofu Dkt Alex Malasusa.
Meneja
wa Tawi la Maendeleo Bank Nuru Shadrack akiwa anaongea na waandishi wa
habari hawapo pichani katika uzinduzi wa bank hiyo iliyozinduliwa na Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa
Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiwa anazindua Maendeleo bank jiji Dar es salaam akianza kwa Maombi ili bank hiyo iwe na neema kwa watumiaji
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Maendeleo bank wakiwa pamoja na wateja waliojitokeza
katika uzinduzi huo jijini Dar es salaam wakiwa tayari kuanza kuweka
pesa zao
…………….
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa amezindua Maendeleo Bank
Kariakoo jijini Dar es salaam huku akitoa pongezi kwa watumishi wa
Kanisa kwa kuweza kuamua kuwasaidia Watanzania katika kuweka pesa zao
katika bank hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali waliohudhulia
uzinduzi huo Askofu Dkt.Alex Malasusa,amesema kuwa ni wakati wa
Watanzania kuacha kufisha pesa nyumbani na kuweka kwenye vibubu kwani
bank hii itaweza kuwasaidia katika kazi zao pindi wanapokuja kuweka pesa
au kuomba mkopa.
“Hii
Maendeleo bank ni ya watu wote haichague dini kwa hiyo mtu yoyote
anweza kufungua Account kwa lengo la kutunza pesa zao na pia amewaasa
watanzania kuwa na nidhamu ya pesa kwani wataweza kufanya shughuli zao
kwa kufuata misingi ya dini pamoja na sheria za nchi”amesema Askofu
Dkt.Alex Malasusa
Kwa
Upande wa Mkurugenzi Mtendaji Mr.Ibrahim Mwangaleba amesema kuwa
Maendeleo bank ni ya watu wote wa dini zote na inawakaribisha wateja
waje kuweka pesa zao katika mahali salama na haitakuwa na ubanguzi
wowote japokuwa ni ya Kikristo.
“Sisi
tumeamua kufungua tawi la Maendeleo bank katika eneo la Kariakoo na
tunaamini kwa imani kuwa hii itakuwa bank kubwa kuliko tawi lolote hapa
jijini Dar es salam na itakuwa bega kwa bega na wateja watakaokuja
kuchukua mkopo kwani hapa Fedha zitakuwa na maombi kwa lengo la wateja
kwenda kuwa na maendeleo ya hali ya juu”amesema Mwangaleba
Post a Comment