Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media group wakati
alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata
katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri
wa Habari utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Mlimani Media wakati alipofanya
ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika
kutekeleza majukumu yao.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia
sehemu mbalimbali za studio za Mlimani Tv na Redio iliyo chini ya
Mlimani Media wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na
changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru Production inayomiliki
vituo vya azam Tv na Redio wakati alipofanya ziara kujionea utendaji
kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia
sehemu mbalimbali za studio za Azam Tv na Redio iliyo chini ya Uhuru
Production wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na
changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
katika Kipindi cha Alasiri Lounge kinachorushwa na Azam Tv iliyo chini
ya Uhuru Production wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake
na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.
………….
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Serikali
imevitaka vyombo vya habari nchini kuwa chachu ya mabadiliko katika
kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchumi wa kati.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses
Nnauye katika ziara yake kwa vyombo vya habari vya Clouds, Mlimani na
Azam, ziara inayolenga kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya Serikali
na vyombo vya habari nchini.
“Serikali
ya Awamu ya Tano imejikita katika ajenda mbalimbali ikiwemo kutoka
katika hali ya uchumi tuliona nao sasa kuelekea uchumi wa kati hivyo
vyombo vya habari vinatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
suala hili linawafikia na kuleta uelewa kwa wananchi”alisema Mhe.
Nnauye.
Waziri
Nape alisisitiza kuwa, kumekuwa na mitazamo tofauti katika vichwa vya
wananchi au jamii kwa ujumla kuhusu suala zima la kuelekea uchumi wa
kati, hivyo ni jukumu la vyombo vya habari nchini kuweza kuwaelewesha
nini maana halisi ya uchumi unaolengwa kuufikiwa.
“tumesikia
ya kwamba uchumi wa nchi umekuwa kwa asilimia saba, mwananchi wa
kawaida hawezi kuwa na uelewa wa kujua ni vipi uchumi wa nchi unakuwa,
hivyo vyombo vya habari vina mchngo mkubwa katika kuifanya jamii kuwa
uelewa juu ya ukuaji wa uchumi” alisisitiza waziri Nape.
Mbali
na hayo Waziri Nape amesema kuwa vyombo vya habari ni chanzo cha
wananchi kuwa kitu kimoja katika kulinda amani ya nchi na utamaduni
uliopo, hivyo vina budi kuzidi kutunza utamaduni uliopo pamoja na
kuwafanya wananchi kupenda utamaduni wao.
Waziri
Nape alisisitiza kuwa vyombo vya habari viifanye jamii kwa ujumla kuwa
na utamadumi hasa wa utamaduni wa ulipaji wa kodi katika nyanja tofauti
na kuwa wazalendo kwa maendeleo ya nchi.
“sisi
kama wanahabari na vyombo vya habari kwa ujumla tunatakiwa kutengeneza
vijana ambao kwao kulipa kodi ni fahari, vijana ambao kazi kwao ni
heshima pamoja na kutengeneza vijana ambao hujivunia uzalendo wa nchi
yao”Alisema Waziri Nape.
Hata
hivyo Waziri Nape ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya
Serikali na vyombo vya habari nchini katika nyanja tofauti ikiwemo
utoaji wa habari muhimu za utekelezaji wa Serikali katika kuleta
maendeleo nchini.
Post a Comment