Rais wa Gambia Yahya Jammeh amekataa
kuondoka madarakani kutoa nafasi ya kuapishwa kwa Adama Barrow hata
baada ya makataa aliyopewa na Senegal kumalizika.
Barrow alipangiwa kuapishwa kuwa rais mpya Alhamisi, na wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi wako tayari kuingilia kati.
Rais
wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz alikutana na Bw Jammeh kwa
mazungumzo ya dakika za mwisho kabla ya kuondoka na kwenda Senegal kwa
mazungumzo na rais Macky Sall.
Bw Barrow
alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu mwezi uliopita na Bw Jammeh
mwanzoni alikubali kushindwa lakini baadaye akapinga matokeo hayo. |
Post a Comment