Waziri wa Habari, utamaduni,
michezo na sanaa Kushoto,Diamond Platnumz katika pamoja na Kaimu
Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania bw.Salum Salum.
Afisa Masoko wa Multichoice
Tanzania Shumbana Walwa akiwa anaongea na waandishi wa habari hawapo
pichani wakati wa kumkabidhi Diamond Platnumz bendera ya Tanzania
kuelekea katika ufunguzi wa Afcon nchini Gabon.
Meneja Masoko wa Multichoice
Tanzania Bw.Alpha Joseph akimkalibisha Kaimu Mkurugenzi Salum Salum
katika hafla ya utoaji wa Bendera kwa msanii wa Bongo Fleva Diamond
Platnumz.
Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice
Tanzania Bw.Salum Salum akimkaribisha mgeni wa tukio ambaye ni Waziri wa
Habari,Utamaduni,Michezo na Sanaa Mh.Nape Nnauye hayupo pichani.
Waziri wa Habri,Michezo,Utamaduni
na Sanaa Mh.Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari wakati wa
kumkabidhi Bendera Diamond Platnumz anayekwenda kwenye shoo ya Ufunguzi
wa Afcon nchini Gabon.
Msanii Diamond Platnumz akitoa
shukruni kwa Serikali na DStv pamoja na waandishi wa habari kwa mchango
wao pamoja na kuendelea kumsapoti kupitia kazi zake.
Mh.Nape Nnauye akisalimiana na Msanii Diamond Platinum.
Msanii wa vichekesho nchini
Tanzania JOTI ambaye pia ni balozi wa Kifurushi cha DStv Bomba ambacho
kitarusha moja kwa moja Michuano ya Afcon akitoa pongezi kwa Kampuni ya
Multichoice Tanzania.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Michezo
na Sanaa Mh.Nape Nnauye katika akiwa na balozi wa kifurushi cha Bomba
Joti kulia pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Bw.Salum
Salum kushoto wakiteta jambo.
Baadhi ya Waandishi waliohudhuria tukio hilo wakiwa katika majukumu yao ya kuchukua picha.
Msanii Diamond Platinum akiwa na
bendera baada ya kukabidhiwa na Serikali tayari kuelekea kwenye ufunguzi
wa Michuano ya Afcon inayoanza Jumamosi ya Januari 14.
Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Nape Nnauye pamoja na Msanii Diamond Platinum.
PICHA NA MO DEWJIBLOG.
………
Kuelekea katika
Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika ‘AFCON’ Kampuni
ya Multichoice Tanzania kupitia Kifurushi cha DStv Bomba imetoa tiketi
sita kwa vijana wa Msanii wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum
kwenda kushuhudia ufunguzi huo.
Ufunguzi huo wa michuano hiyo mikubwa Afrika, inatarajiwa
kufanyika Januari 14, mwaka nchini huko ambako Dimaond amealikwa kwenda
kutuimbuza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Nape Nnauye alimkabidhi bendera ya taifa, Diamond kwa ajili ya kwenda
kuipeperusha vyema Tanzania katika ufunguzi huo.
“Kikuweli nimpongeze Diamond kwa mwaliko
alioupata wa kwenda kutumbuiza kwenye michuano mikubwa Afrika ya Afcon,
siyo kitu kidogo kwake, ni nafasi ya yeye kujitangaza zaidi kimataifa,
ninaamini wapo wasanii wengi wazuri Afrika, lakini kachaguliwa yeye
hivyo anastaili pongezi,” alisema Nape.
Nape ndiye aliwaomba
DStv kujitokeza na kudhamini safari ya wachezaji shoo wa Diamond na
baadhi ya watu wa timu yake kwenda Afcon ili kuhakikisha anafanya shoo
ya uhakika zaidi.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DStv, Salum Salum
alisema wametoa tiketi hizo kwa Diamond kwa lengo kukuza na kuendeleza
vema tasnia ya filamu.
“Tunathamini tasnia
ya sanaa nchini kwa kupitia muziki na filamu, hivyo basi katika kutambua
hilo tumetoa tiketi sita kwa kundi la WCB chini ya msanii Dimaond kwa
ajili ya kwenda kwenye uzunduzi wa Afcon huko Gabon.
“Tumempatia tiketi hizo, baada ya kuomba
udhamini wa tiketi hizo kwa ajili ya vijana wake sita atakaombatana nao
kwenye shoo hiyo na kikubwa tunataka kuona Diamond anafunika ili
atauwakirishe vema,” alisema Salum.
DStv, ndiyo itaonyesha michuano hiyo mikubwa ya
kimataifa kwa kifurushi chake cha bei cha chini kabisa kitakachopatikana
kwa Shilingi 19, 975 tu.
Post a Comment