Chuo
cha Kodi kitafanya mahafali ya Kumi Jumamosi tarehe 18 Novemba 2017
katika ukumbi wa chuo cha Kodi ambapo Mgeni rasmi katika mahafali hayo
anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
Katika
mahafali hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mpango atatunuku vyeti,
stashahada na shahada kwa wahitimu 520 ambao wamefuzu masomo yao mwaka
2016/2017 na kusathili kutunukiwa vyeti.
Dkt.
Mpango pia atatoa zawadi mbalimbali kwa wahitimu 12 waliofanya vizuri
zaidi katika masomo ikiwa ni utaratibu ambao chuo kimejiwekea ili
kutambua jitihada nzuri ambazo zimefanywa na wanafunzi hao pamoja na
kuwashajihisha wanafunzi wanaoendelea na masomo kufanya vizuri zaidi
katika masomo.
Jumla
ya anafunzi watakao tunukiwa vyeti, stashahada na shahada katika
mahafali ya Kumi ya Chuo cha Kodi ni wahitimu 82 wa Cheti cha Uwakala wa
Forodha cha Afrika Mashariki yaani the ‘East African Customs and
Freight Forwarding Practising Certificate (EACFFPC). Wahitimu 39 wa
Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani ‘Basic Technician
Certificate in Customs and Tax Management (CCTM). Stashahada ya
Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani ‘Diploma in Customs and Tax
Management – (DCTM)’ wahitimu – 147, Shahada ya Usimamizi wa Forodha na
Kodi yaani ‘Bachelor of Customs and Tax Management (BCTM)’ Wahitimu –
134, ‘East African Community Postgraduate Certificate in Customs
Administration (PGCCA)’ wahitimu 85 na Stashahada ya Uzamili katika Kodi
yaani ‘Postgraduate Diploma in Taxation (PGDT) wahitimu - 33
Pamoja
na kutunuku vyeti stashahada, na shahada kwa wahitimu, Mgeni Rasmi pia
atatoa tuzo kwa wahadhiri wa Chuo cha Kodi waliofanya tafiti mbalimbali
katika kipindi cha mwaka wa masomo wa 2016/2017 na kuchapishwa katika
majarida mbalimbali ya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na jarida la Chuo cha
Kodi yaani ‘Journal of the Institute of Tax Administration’ (JITA).
Vilevile
Chuo cha Kodi kinasherehekea miaka kumi tangu kipate ithibati (usajili)
kutoka Baraza la Taifa la Vyuo vya Ufundi (NACTE).Chuo
cha Kodi kinajivunia miaka kumi ya mafanikio katika kutoa mafunzo ya
Forodha na Kodi yanayokidhi soko la ajira katika nyanja za forodha na
Kodi ndani na nje ya nchi.
Tangu
kipate usajili wa kudumu kutoka Baraza la Vyuo vya Ufundi (NACTE), Chuo
kimepanua wigo wa taaluma kutoka kutoa mafunzo kwa watumishi wa TRA
pekee hadi kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa masuala ya forodha na
kodi kwa nchi za Mashariki Kati na Kusini mwa Afrika.
Kikiwa
katika hatua za mwisho za utekelezaji wa Mkakati wa Tatu, Chuo cha Kodi
kinaendelea na maandalizi ya kuwa Kituo cha Umahiri wa Forodha na Kodi
katika Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Sekretarieti ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki kukiteua Chuo cha Kodi kuwa Kituo cha Umahiri Afrika
Mashariki
Nachukua
fursa hii kuwakaribisha wahitimu pamoja wageni waalikwa wote pamoja na
nyinyi waandishi wa habari katika mahafali haya ya Kumi yatakayofanyika
katika Ukumbi wa Multipurpose Chuo cha Kodi tarehe 18 Novemba 2017
kuanzia saa tatu asubuhi.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Prof. Isaya J. Jairo
MKUU WA CHUO
Mkuu
wa Chuo cha Kodi (ITA,) Profesa Isaya Jairo akiongea na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo kuhusu mahafali ya kumi ya chuo hicho
yanayotarajiwa kufanyika chuoni hapo Jumamosi Novemba 18 2017. Kushoto
ni Afisa Uhusiano Mkuu wa chuo, Oliver Njunwa. (Picha na Robert Okanda
wa Okanda blogs)
Mkuu
wa Chuo cha Kodi (ITA) Profesa Isaya Jairo akiongea na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo kuhusu mahafali ya kumi ya chuo hicho
yanayotarajiwa kufanyika chuoni hapo Jumamosi Novemba 18 2017. Kulia ni
Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo (Utawala), Emmanuel Masalu na Afisa Uhusiano
Mkuu wa chuo, Oliver Njunwa.
Post a Comment