Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto
Dkt Mpoki Ulisubisya akizungumza na menejimenti ya MOI (hawapo pichani)
katika ukumbi wa Mikutano wa MOI.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya akimjulia hali mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji
mkubwa wa mgongo, anayetoa ufafanuzi wa namna upasuaji huo ulivyofanyika
ni Dkt. Nicephorus Rutabansibwa (Daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo
na Mgongo). Kushoto ni Mganga mkuu wa Serikali Profesa Muhamed Kambi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto
Dkt Mpoki Ulisubisya akikagua mashine mojawapo katika benki ya damu ya
MOI.
Mtaalamu
wa Maabara Bwana Mbuta Jackson akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki
Ulisubisya kuhusu namna benki mpya ya damu inavyofanya kazi kwa
kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu salama.
Watumishi
wa MOI wakifuatilia hotuba ya katibu Mkuu Wizara ya Afya ,Maendeleo ya
Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto ( Sekta ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya
(hayupo pichani) katika ukumbi wa Mikutano MOI.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto
Dkt Mpoki Ulisubisya akitoa maelekezo alipokua anakagua maeneo ya utoaji
huduma katika jingo jipya la MOI (MOI phase III).
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya ( katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na
menejimenti ya MOI.( Picha zote na MOI ).
……………………………………………………………………………..
Patrick Mvungi- MOI
Taasisi
ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu
(MOI) imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kusafirisha
wagonjwa nje ya nchi kufuata matibabu baada ya MOI kuanzisha huduma za
kibingwa ambazo awali zilikua hazipatikani hapa nchini.
Hayo
yamebainishwa katika ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii , Jinsia Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alipotembelea MOI
na kukagua hali ya utoaji wa huduma, mazingira , miundombinu na
kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kukutana na menejimenti.
Akizungumza
na menejimenti ya MOI, Dkt. Ulisubisya amepongeza kazi nzuri na kubwa
inayofanywa ambayo imepelekea watanzania kupata huduma bora za kibingwa
ambazo wangepaswa kuzifuata nje ya nchi.
“Mnafanya
kazi nzuri sana, jambo ambalo linatupa faraja kubwa sisi viongozi wenu,
naomba muongeze ubunifu zaidi, hamtakiwi kuifikiria MOI kwenye ukanda
huu wa Afrika pekee bali duniani, hii ni changamoto kwetu sote
kuifikisha hapo ”alisisistiza Dkt. Ulisubisya
Aidha,
Dkt Ulisubisya amesema MOI imepunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa
asilimia 95% na asilimia 5% iliyobaki MOI inaweza kuimaliza kabisa na
kusiwepo mgonjwa wa kwenda nje ya nchi.
Pia,
amewaelekeza viongozi wa MOI kushirikiana na Wizara ya Afya kutafuta
namna ya kufuta rufaa kwa kutoa mapendekezo na ushauri utakaosaidia
kutatuliwa kwa changamoto hiyo.
“Azma
ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe
Magufuli ni kuhakikisha huduma zote za Afya zinapatikana hapa nchini na
vyema sote tukamuunga mkono” amebainisha Dkt. Ulisubisya.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhamed Kambi amepongeza
uongozi wa MOI kwa kuwa na maono ya mbali ya kuifanya MOI kuwa Taasisi
bora barani Afrika na Duniani.
“Nimefurahi
kwamba MOI mna maono ya mbali, mnafikiria kuitoa Taasisi hii hapa ilipo
na kuifikisha sehemu ya juu zaidi, dira yenu ni kuwa Taasisi bora
Afrika kufikia 2022 fanyeni kazi kwa bidii kufikia lengo hilo.” amesema
Prof Muhamad Kambi
Awali
akiwasilisha taarifa ya Utendaji, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt
Respicious Boniface amesema toka kuanzishwa kwa Taasisi hiyo imefanikiwa
kuanzisha huduma za kibingwa za Upasuaji wa Nyonga, Magoti, Ubongo,
Mgongo, Vibiongo, Usingizi ambazo zimesaidia kupunguza rufaa za nje ya
nchi.
“Baada
ya kuanzisha huduma hizi za Kibingwa tumefanikiwa kuokoa shilingi
Bilioni 5 ambazo zingetumika kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi,
tumepunguza rufaa kwa asilimia kubwa naomba nikuhakikishie hata hizi
asilimia 5% zilizobaki tutashirikiana na Serikali na naamini zitakwisha
kabisa.” amesema Dkt. Respicious Boniface.
Post a Comment