Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea
vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo
jijini Dar es salaam .
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy
Mwalimu (kulia) akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani ya
kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw.
Jeremia Zoungran (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa vya
kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
(kulia) akipokea moja ya nyenzo za kufundishia juu ya uchunguzi wa
saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini
Tanzania Bw. Jeremia Zoungran (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa
vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam katikati ni
Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .
Mkurugenzi
Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran akiongea na
waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya
kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini
Dar es salaam .
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy
Mwalimu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji
wa Wizara ya afya, Jpiego na USAID wakati wa kupokea vifaa vya
kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini
Dar es salaam wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini
Tanzania Bw. Jeremia Zoungran na aliyevaa nguo ya pundamilia ni Afisa
Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .picha na Emmanuel
Massaka,Globu ya jamii.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
WAZIRI
Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
amewaelekeza waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuanzisha zoezi la wazi
la uchunguzi wa saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili
kusaidia kutokomeza tatizo kwa wanawake hilo nchini.
Hayo
amesema wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani
ya shilingi milioni 98 ambavyo vimetolewa na Taasisi isiyo ya
Kiserikali ya JHPIEGO kwa kushirikiana na USAID ili kusaidia kupambana
na tatizo hilo nchini.
“Angalau
ifikapo Desemba 2018 nataka vituo vya Afya vya Serikali 524 viwe
vinatoa huduma ya matibabu ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi na
kufikia wanawake milioni 3 watakaopata huduma hii ili kuokoa wanawake
wa vijijini kwani mpaka sasa hivi tunavyo vituo vya afya 265
vinavyotoa huduma hii ” alisema Waziri Ummy.
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa uchunguzi na kutoa chanjo ya Saratani ya
mlango wa kikazi kwa wasichana kuanzia miaka 9 mpaka 14 ili kuweza
kupunguza vifo vitokanavyo na tatizo hilo kwani katika kila wanawake 100
vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ni 32.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika kuongeza jitihada za kupambana
na ugonjwa huo Serikali imeongeza vituo vya afya 100 kutoka 343 hadi
kufikia 443 mwaka huu ili kutokomeza tatizo hilo nchini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia
Zoungran amesema kuwa walianzisha mpango wa kupambana na tatizo hilo na
kufanikiwa kuwafikia wanawake elfu 75 kwa mikoa 4 tangu mwaka 2009.
“Mbali
na mikoa hiyo 4 bado tunalengo la kuongeza mikoa mingine 7 ili kuweza
kutoa huduma hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Juhudi za Serikali katika
kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi ili kuweza kuokoa wanawake
wengi zaidi nchini” alisema Bw. Zoungran.
Post a Comment