Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Wachezaji
wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa
Tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake
ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akimkabidhi Bendera ya
taifa Nahodha wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la
Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya
Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni
Mwenyekiti
wa wa Chama cha Gofu nchini Joseph tango (Aliyesimama) akizungumza
wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari makao makuu ya jeshi Upanga
ambapo Timu ya Wanawake ya Klabu ya jeshi ya Lugalo walikabidhidhwa
bendera kwa Ajili ya kushiriki Michuano ya Wazi nchini Nigeria aliyeka
Kushoto ni Mwenyekii wa Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo
Mstaafu.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika Picha ya
Pamoja na Wachezaji na Viongozi wa Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la
Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Wakuu wa Matawi na Wachezaji wanaotarajia
kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi
karibuni (Picha na Luteni Selemani Semunyu
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewataka wachezaji wa Timu
ya Wanawake ya Gofu ya Klabu ya Jeshi ya Lugalo kuhakikisha wanarejesha
heshma ya jeshi kuwa kinara katika michezo na kuzalisha wachezaji bora
wanaowakilisha nchi kwa mafaniko.
Aliyasema
hayo Makao Makuu ya jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam wakati akiagana
na wachezaji Sita wa Gofu wanaotarajia kuwakilisha nchi katika michuano
ya wazi ya wanawake nchini Nigeria IBB Ladies Open Championship 2018
yanayaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Jenerali
Mabeyo alisema kama ilivyokuwa katika Michezo ya Riadha na Ngumi sasa
tunataka na kwenye gofu na kwa kuanza ni timu hii ya Gofu ya Wanawake
kuhakikisha inarudi na ushindi mnono.
“
Nikiwa mlezi wa Klabu naamini mtatuwakilisha vyema na Jeshi kwa ujumla
tutaendelea kuwaunga mkono wachezaji wa Gofu na hata Michezo mingine
kuhakikisha jeshi linaendelea kuwa kinara w michezo nchini na kuwa
chachu kwa wengine” Alisema Jenerali Mabeyo.
Aliongeza
kuwa licha ya matumaini yake katika Gofu lakini pia katika Soka licha
ya Mchezo huo kutawaliwa na simba na yanga lakini sasa walau mwanga
unaonekana baada ya ya Timu ya Jeshi ya Green Worriorrs kuifurusha Timu
ya Simba katika Michuano ya Kombe la Shirirkisho.
“Ushindi
ule ulikuwa Mwanzo mzuri wa kupunguza Ubabe wa Simba na Yanga na
Ushabiki wa Simba na Yanga hata miongoni mwa Wachezaji hivyo nanyi kama
mlivyofanya vyema katika mashindano Uganda sasa tunatarajia Ushindi toka
Nigeria” Alisema Jenerali Mabeyo.
Kwa
Upande wa mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo
Mstaafu aliwataja wachezaji hao kuwa ni Nahodha Ayne Magombe, Sara Denis
, Sophia Mathius ,Hawa Wanyenche ,Christina Charles na Angel Eaton huku
mkuu wa Msafara akiwa ni Kapten Japhet Masai.
“ Nina
matumaini makubwa na Kikosi hiki tunachokituma Nigeria naamini
kitarejesha furaha kwa Klabu ,jeshi na Watanzania kwa ujumla ukizingatia
uwezo Binafsi wa Wachezaji Mazoezi na Historia kutokana na michuano
iliyotangulia” Alisema Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo.
Kwa
Upande wake mwenyekiti wa Chama cha Gofu nchini TGU Joseph tango
amelipongeza jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania kwa jitihada katika
kuendeleza michezo hasa mchezo wa gofu ambao klabu ya Lugalo imekuwa
kielelezo.
Aliomba
mkuu wa majeshi ya ulinzi na Mlezi wa Klabu ya Lugalo kuendelea
kuisaidia Klabu hiyo ambayo ndio klabu yenye mashindano mengi kwa mwaka
ukilinganisha na Klabu nyingine nchini ikiwemo kusaidia utekelezaji wa
Ujenzi wa Uwanja makao makuu ya nchi Dodoma.
Mashindano
hayo ya Siku Tatu yanatarajiwa kuanza Tarehe Nane Februari huku
wachezaji kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,Uganda, Zambia na Malawi
wakitarajiwa kushiriki.







Post a Comment