Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla (mwenye miwani) akimkabidhi mti wa matunda  mmoja wa wananchi waliojitokeza katika  hafla ya uzinduzi wa upandaji miti  Kimkoa  katika Kata ya Iganzo Jijini Mbeya

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Iganzo jijini Mbeya wakiwa wameshika miti ya Matunda tayari kwa zoezi la upandaji katika chanzo cha maji cha mto Imeta  barabara ya Mbeya Chunya .

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipanda mti kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti kimkoa barabara ya Mbeya Chunya ambapo katika zoezi hilo mkuu huyo wa mkoa aliwataka wananchi kuepuka  kilimo na makazi kandokando ya mito ,vyanzo vya maji na maeneo yote ya hifadhi.

Askari wa Jkt wakishiriki vyema zoezi la upandaji miti katika katika ya Iganzo katika chanzo cha Maji cha Mto Imeta jijini Mbeya.


Zoezi la Upandaji miti likiendelea


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top