Na EmanuelMadafa
Michuzi Blog -MBEYA.
Jeshi la
Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mkazi wa kijiji cha Isutu Kata ya Ilongo
Wilayani Mbarali Geofrey Emilo kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa miezi mitano Prince Geofrey kisha kuufukia mwili wake porini.
Kaimu Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Modestusi Chambu, alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka
kwa mashahidi mbalimbali, inadaiwa kuwa mtuhumiwa alimuua mtoto huyo kwa kumnywesha
sumu ambayo bado haijafahamika aina yake na kwenda kumfukia porini.
Kwa mujibu wa
Kamanda Chambu, alisema tukio hilo limetokea Agosti 28 mwaka huu katika Kijiji
cha Isitu porini, Kata ya Chimala, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa
Mbeya
Ambapo baba
mzazi huyo alikwenda nyumbani kwa mtalaka wake mke baada ya kutengana na
kumchukua mtoto huyo kwa nguvu bila kibali cha mama mzazi wa mtoto.
.
Alisema,
Agosti 30, mwaka huu mtuhumiwa alikamatwa na alipohojiwa alikiri kuwa mtoto
huyo amemuua na kumtupa porini na katika ufuatiliaji aliwapeleka askari eneo
alipokuwa amemfukia marehemu.
“Chanzo cha
tukio hili ni wivu wa kimapenzi kwani mtuhumiwa alikuwa anahisi mtoto huyo sio
wake amebambikiwa ni wa mwanaume mwingine,”alisema.
Katika tukio
lingine polisi Mkoani Mbeya, linawasaka watu wanaodaiwa kufukua kaburi na kisha
kuchukua mifupa ya mwili wa marehemu ambaye alikuwa na ulemavu wa ngozi
(Albinism).
Tukio hilo
limetokea tarehe 30.08.2018 majira ya saa 03:00 usiku huko katika Kijiji cha Ngonga,
Wilaya ya Kyela, Mkoa wa mbeya ambapo kaburi la mtu mmoja aliyekuwa anajulikana
kwa jina la Andusamile Mwalwebe (65) Mkazi wa kijiji cha Ngonga ambaye
aliyefariki dunia mwaka 2012 kwa maradhi ya kawaida.
Kaimu Kamnada
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Modestusi Chambu, alisema kaburi la mlemavu huyo wa
ngozi, lilikutwa limefukuliwa na mtu/watu wasiojulikana na kisha watu hao
kuchukua mifupa ya mwili wa mtu huyo ( skeleton) a kwamba kiini cha tukio hilo
ni imani za kishirikina.
Mwisho.
Post a Comment