Na EmauelMadafa
, Michuzi Blog , MBEYA.
MIGOGORO ya wazazi katika familia, imetajwa kuwa ni
moja ya sababu kubwa inayoathiri elimu na malezi bora ya watoto.
Kauli hiyo imetolewa jijini Mbeya na Afisa
Utawala Shule za St.Mary's Mkoa wa Mbeya, Anuciata Ngonyani kwenye mahafali ya
wanafunzi 63 wa darasa la saba.
Amefafanua kuwa uongozi wa shule hiyo umekuwa
ukipokea kesi nyingi za namna hiyo, hivyo kuwaomba wazazi wakiume kutambua
wajibu wao kwa watoto ikiwa na kuwatendea haki kwa kutimiza haki zao za msingi
ikiwemo elimu.
Aidha, amewataka wazazi kujenga mshikamano, umoja, amani na
upendo kwenye familia ili watoto waweze kuiga mambo yaliyomema na kukua katika
maadili.
Amesema kuna watoto wengi wameacha masomo na
wengine kuhamishwa shule kutokana na jukumu la kusomesha mtoto kuachiwa mama pekee jambo hali ambayo imekuwa ikimnyima haki mtoto. .
Kwa upande wake Meneja wa bima Kanda ya Nyanda
za Juu Kusini Consolatha Gabone amesema moja ya changamoto zinazo poteza ndoto za watoto ni
mifarakano ndani ya familia hasa pale wazazi wanapo tengana au kufariki.
Amesema kutokana
hali hiyo wameamua kuanzisha huduma ya bima ya maisha ambayo inatoa fursa kwa
wategemezi kutimiza ndoto zao bila kuathiri mfumo wa maisha licha ya kuondokewa
na wazazi.
Gabone amesema kuwa imekuwa ni jambo la
kawaida kwa wazazi kuwa na bima za magari na mali nyingine na kusahau bima za
maisha ikiwemo elimu ambayo ni njia ya kumwezesha mwanafunzi kufikia ndoto zake
kabla ya kuanza kujitegemea.
Amesema ili kuweza kuonyesha upendo kwa watoto ni
vema wakafungua bima ya elimu ili kuweza kutimiza malengo ya watoto.
Wengi wamesau kwa habari ya maisha yao wenyewe unajua mzazi anapo kuwa amekata bima ya
maisha ni kuonyesha upendo kwa familia lakini kuna wakati unaweza kupata
madhara hivyo ukashindwa kusomesha lakini ukakata bima hasa ya elimu watoto
wataendelea na masomo hivyo niwashuri wazazi kukata bima ili kuwezesha kutimza
malengo ya watoto wao’alisema Gabone
Afisa Utawala Shule za St.Mary's Mkoa wa Mbeya, Anuciata Ngonyani akizungumza kwenye mahafali ya wanafunzi 63 wa darasa la saba. |
Rose Lwakatare (Mtoto wa Mchungaji Mama Lwakatare ) akizungumza katika sherehe hizo zilizofanyika shuleni hapo . |
Meneja wa bima (TIRA)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Consolatha Gabone akizungumza katika mahafali hayo |
Wanafunzi wakitoa burudani katika sherehe hizo. |
Wazazi na Walezi ambao walipata fursa ya kuhudhuria sherehe hizo |
Post a Comment