Na EmanuelMadafa,Mbeya
MAKAMU wa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia
Suluhu, amewahakikishia wakazi wa Mkoa wa Mbeya, kwamba serikali imejipanga
kutekeleza na kutatua changamoto muhimu za kimaendeleo, ikiwemo ya miundombinu
ya barabara.
Makamu wa Rais, ameyasema hayo, leo wakati akizungumza na
mamia ya wananchi katika eneo la Mbalizi Wilayani Mbeya, eneo linalotajwa
kuongoza kwa matukio ya ajali za barabarani.
Amesema, katika kulitekeleza hilo, tayari serikali
imeshughulikia changamoto ya ujenzi wa barabara ya mchepuko ya kilomita 40
ambayo itasaidia kupunguza au kudhibiti ajali za barabarani zinazotokea kwenye
barabara kuu ya Tanzania na Zambia (TAZAMA).
“Mwaka juzi
mlifanya kazi kubwa sana, tumekuja kuwahikikishia kwamba serikali itatekeleza
yale yote tuliyo ahidi, nadhani spidi mnaiona,”amesema.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani kwani
ndio sialaha ya maendeleo na kuwasisitiza kuchaguai viongozi watakaoendana na
kasi ya rais na waioendekeza tama wakati wa uchaguzi wa viongozi wa serikali za
mitaa.
Mwisho.
Post a Comment