Meneja wa Timu Ndugu Boniface Clemence akizunguzia juu ya maendeleo ya Kambi hiyo |
Na Madafa Emanuel,Tukuyu
KIKOSI cha Wachezaji 33 Cha timu ya maboresho ya Taifa Stars,
kimeendelea vyema katika kambi yake
iliyoko Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani mbeya katika Hotel ya Land Mark Hotel.
Uwanja unaotumika na wachezaji hao kwa jaili ya mazoezi ni katika Chuo Cha Ualimu Cha Msasani kilichopo hatua
kadhaa toka katika Hotel hiyo.
Akizungumza na Blog hii
Meneja wa Timu hiyo Ndugu Boniface Clemence amesema kuwa kambi ya vijana hao
inaendelea vyema licha ya kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.
Amesema kwa asilimia kubwa vijana hao wapo katika afya njema
hasa kutokana na kupatiwa huduma nzuri zilizopo kambini hapo.
Amesema vijana hao
wameonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa kuonyesha ushirikiano kutoka kwa
viongozi wao.
Hata hivyo Kocha Mkuu
Ndugu Oscar Koloso amesema kuwa maendeleo ya vijana hao yako vizuri licha ya
kukumbana na hali ya hewa yenye baridi kali hali ambayo imewafanya baadhi yao
kuteteleka kidogo hasa kutokana na mazingira waliyotoka.
Amesema changamoto kubwa
wanayokabiliana nayo ni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kila siku hali
ambayo inawafanya wafanye mazoezi na mvua hizo huku siku nyingine kulazimika
kufanya mazoezi ya kukimbia tu badala ya kuimgia uwanjani.
Amesema kwa sasa wapo
katika hatua ya kufanya mazoezi magumu ya kukimbia na mpira kwani mazoezi
magumu ya viongo wamekwisha kamilisha.
Hata hivyo Kocha huyo
amebainisha kuwa wamejaribu kwenda haraka hasa kutokana na muda kuwa mchache
katika kambi hiyo ambayo kwa hatua ya kwanza wanatakiwa kukaa kwa kipindi cha
mwezi mmoja.
Wachezaji waliobahatika
kuingia kwenye mchakato huo wa maboresho ya Taifa Stars kuwa ni Abdulaziz Khatib Haji (Mjini Magharibi),
Abubakar Abbas Ibrahim (Tanga), Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara) na Mtindi Kheri
Ali (Kaskazini Unguja) ambao ni makipa.
Kwa upande wa mabeki wa
pembeni waliochaguliwa katika mchakato huo ambao upo chini ya udhamini wa
Kilimanjaro Premium Lager ni Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Hussein
Moshi (Tabora), Omari Kindamba (Temeke) na Shiraz Abdallah (Ilala).
Mabeki wa kati ni Abbas
Ali Haji (Kaskazini Unguja), Ancy Abdon (Kagera), Emma Namwamba (Temeke),
Hussein Juma Akilimali (Njombe), Joram Nasson (Iringa), Kayombo Silvanus
Henrico (Ilala), Miraji Maka (Mwanza), Ramadhan Ame Ramadhan (Kusini
Unguja) na Said Juma Ali (Mjini Magharibi).
Viungo wapo Abubakar
Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magoma (Shinyanga), Juma Said
Jega (Lindi), Mtenje Alban Juma (Tanga), Ryna Mgonyike (Temeke) na Yusuf
Mpilipili (Temeke).
Washambuliaji ni Abdallah
Kagumbwa (Temeke), Abrahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Athanas Fabian
Bayagala (Mbeya), Athanas Mdamu (Mwanza), Ayubu Hashim Lipati (Ilala), Chunga
Said (Manyara), Mbwana Mshindo Mussa (Tanga), Michael David Mlekwa (Lindi),
Mohamed Seif Said (Kusini Pemba), Omar Athuman Nyenje (Mtwara), Paul Michael
Bundala (Ilala), Ramadhan Kapalamoto (Kinondoni) na Roman Nyapunda (Temeke).
Chuo cha Ualimu Cha Msasani ambacho uwanja wake unatumikam kwa vijana hao |
Post a Comment