Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Ndugu Chrispin Meela |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Halimashauri
ya Wilaya Rungwe Mkoani Mbeya iko katika mchakato wa haraka wa namna ya kuweka
soko la uhakika la zao la ndizi.
Mkuu wa
Wilaya hiyo Chrispian Meela akizungumza wilayani humo k amesema umefika wakati
sasa wakulima wa zao la Ndizi wakaanza kunufaika na zao hilo pamoja na
halimashauri kupata mapato .
Amesema kwa
muda mrefu sasa wakulima hao wamekuwa wahawanufaiki na zao hilo hutokana na
kutokuwepo kwa soko la uhakika huku wachache wakiendelea kunufaika.
Kufuatia
hali hiyo Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa mpango uliopo sasa ni kuzungumza na
Halmashauri za Kinondoni ,Ilala na Temeke kwa lengo la kutenga eneo moja kwa ajili ya kufanyia
biashara hiyo.
Amesema hivi
karibuni itaundwa timu ya madiwani wa
halimashauri hiyo ambao wataungana na baadhi ya wataalamu na kufanya ziara
jijini Dar es salaam kwa lengo la
kufanikisha zoezi hilo .
Amesema
kuungana kwa Halmashauri hizo kutasaidia kupatikana kwa soko la uhakika pamoja
na halmashauri hiyo kupata fedha za uhakika kutokana na ushuru utakao patikana
katika zao hilo pamoja na kudhubiti bei.
Kwa Muda
mrefu sasa biashara ya ndizi imekuwa ikifanyika kiholela huku wakulima
wakiendelea kuwa maskini.
MWISHO.
Post a Comment