Moja ya Miradi ya Maji ianyotekelezwa na Halmashauri hiyo ya Rungwe. |
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Ndugu Chrispian Meela |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
MIRADI ya maji katika
halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, imeshindwa kutekelezwa kwa miaka
mitano kutokana na watendaji wa halmashauri hiyo kutowashirikisha
madiwani husika.
Hali hiyo
imejitokeza kwenye kikao cha Baraza la
Madiwani la Halmshauri hiyo wakati wakijadili taarifa ya serikali ya
utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya
Rungwe Chrispin Meela.
Akitaja baadhi ya
miradi hiyo, Meela alisema kuwa ni mradi wa maji wa Masoko na Kimo ambayo
licha ya serikali kuwasilisha fedha zake kwa wakati lakini imeshindwa
kutekelezeka.
Amesema, mradi
wa maji wa Masoko ambao ulitengewa shilingi Bilioni moja mwaka 2009
na kutakiwa kukabidhiwa kwa halmashauri mwezi Desemba
2012 lakini ulishindikana kutokana na serikali kusitisha mkataba wake baada
ya kubaini kuwa mkandarasi huyo aliwasilisha nyaraka feki wakati wa
ushindanishi wa tenda.
“Mkandarasi huyu wa
Kampuni ya OSAKA STORE aliidanganya serikali ya kwamba kampuni yake
imekidhi vigezo na masharti katika ushindani wa tenda pamoja na kuwasilisha
nyaraka za uongo za akaunti yake ya fedha,”amesema.
Kutokana na hali hiyo,
Meela aliwataka Madiwani kuwa makini kwenye mikataba pamoja na kutoruhusu
mikataba inayohusu miradi ya maendeleo kusainiwa ofisini kwa kushirikisha
watendaji pekee.
Akichangia hoja hiyo
Diwani wa Kata ya Makandana, Boniface Mwasikili ameonesha kushangazwa na
taarifa hiyo huku akihoji ya kwamba ni kwanini uongozi wa halmashauri
ulishindwa kuwashirikisha madiwani hususani kamati husika.
“Haiwezekani mkandarasi
apewe mradi wa mamilioni ya fedha pasipo shirikisha kamati
husika,huu ni utapeli ambao unaonekana kufanywa na baadhi ya watumishi
,”alisema .
Amesema, kitendo cha
watendaji kuingia mkataba na mtu ambaye hawajamfanyia uchunguzi wa kustosha ni
uzembe na kwamba hatua za kinidhamu zikachukuliwa dhidi yao.
Hata hivyo Baraza hilo
limeadhimia kuchukuliwa hatua kwa watumishi wote ambao watabainika kushiriki
kwenye udanganyifu huo huku wakiuagiza uongozi wa halmashauri kumfikisha
mahakamani mkandarasi huyo.
Mwisho.
Post a Comment