Mkuu wa Wilaya Chunya Deodatus Kinawilo |
Hii ndio Zahanati iliyofungwa kutokana na kutokuwepo kwa mtoa huduma Katika Kijiji cha Gua Kata ya Gua Wilayani Chunya Mkoani Mbeya. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
WANANCHI wa Kata ya Gua
iliyopo Wilayani Chunya, Mkoani Mbeya, wameilalamikia serikali kwa kushindwa
kupeleka watumishi kwenye Zahanati ya afya hali iliyopeleka kufungwa kwa
jengo hilo na wao kukosa huduma.
Zahanati hiyo imefungwa
kwa zaidi ya mwezi mmoja kwa kile kinachosemekana mkunga aliyekuwepo kwenda
likizo ya mapumziko.
Wakizungumza na Blog hii
hii wakazi wa Kijiji cha Gua Kata ya
Gua, walisema huduma kwenye Zahanati hiyo ilianza kusuasua kuanzia
mwezi January mwaka huu na ulipofika mwezi February ndipo waliposhangaa kuona
jengo hilo limefungwa.
“Kipindi cha nyuma
huduma ilikuwa ikitolewa kwa kusuasua, lakini hivi karibuni ndio
tumeshangaa kukuta jengo hili likiwa limefungwa na tulipofuatilia kwenye
uongozi wa serikali ya kijiji tumeambiwa kuwa muuguzi aliyekuwepo ameenda
mapumziko,”alisema Krispin Mikael mkazi wa Gua.
Amesema, awali
Zahanati hiyo ilikuwa na mganga aliyetajwa kwa jina moja la Semwenza
ambaye alistaafu na kijiji kukaa zaidi ya miaka miwili bila ya mganga
hivyo kuendeshwa na mkunga tu.
Amesema, tatizo
kubwa ni pale mkunga huyo anapopatwa na matatizo pamoja na kuchukua likizo ya
mapumziko hivyo jengo hilo la Zahanati hufungwa na kumsubili mpaka siku atakapo
rejea ofisini.
Amesema imefika wakati wanajiona kama wao sio watanzania kutokana na kuwepo kwa hali hiyo
Amesema imefika wakati wanajiona kama wao sio watanzania kutokana na kuwepo kwa hali hiyo
Amesema, katika kipindi
chote hicho wagonjwa huendelea kuteseka kwa kutembea
umbali mrefu kwenda kutafuta huduma na wengine huishia kwa waganga wa kienyeji.
Amesema, baadhi ya
wagonjwa hukimbilia kwa waganga wakienyeji kutibiwa ambao wengi wao
hutumia ramli za uchonganishi na kusababisha migogoro isiyokuwa na ulazima
ndani ya jamii.
Aidha, jitihada za
kumtafuta Mwenyekiti wa Kijiji hicho kwa nia ya kupata maelezo ya jambo hilo
ziligonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa kiongozi huyo alikuwa amesafiri kikazi.
Mkurugenzi Halmashauri ya Chunya
Sophia Kumbuli ambaye aliahidi kulifanyia kazi tatizo hilo ikiwa ni
pamoja na kufika kwenye eneo la tukio.
Mwisho.
Post a Comment