Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



Bado idadi kubwa ya wananchi na wakazi wa jiji la Mbeya ambao wamekuwa wakipata huduma katika hospital ya Rufaa Mbeya wamekuwa na uelewa tofauti juu ya zoezi zima la unawaji mikono mara baada ya kumaliza kuhudumiwa katika hospital hiyo.

Hata hivyo licha ya uongozi wa hospital hiyo kuendelea kuweka msisitizo juu ya suala hilo bado uelewa wa wananchi hao umekuwa mdogo zaidi.


 Blog hii ilifanikiwa kutembelea eneo hilo la hospital ya Rufaa Mbeya kujionea hali halisi ya juu ya wateja wa hospital hiyo namna wanavyo itikia katika suala zima la unawaji mikono kama taratibu za kiafya zinavyotaka.

Hivyo kutokana na hali hiyo nipende kutoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali mkoani hapa kuhakikisha wanaendelea kuhamasishana katika zoezi zima la unawaji mikono mara wanapo toka katika hospitali hiyo kutibiwa au kuangalia wagonjwa kwa lengo la kulinda na kutunza afya zao
Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top