Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kamanda wa Polisi Mbeya Ahmed Msangi
Na EmanuelMadafa

Jeshi la Polisi Mkoani linamshikilia Mkazi wa kijiji cha Lusungo Wilayani Kyela Mkoani Mbeya Ndugu Obedi Makupa(37 )kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga mwenye umri wa siku tano aitwaye David Semen.
Tukio hilo limetokea June27 mwaka huu  majira ya saa 04:00 alfajiri katika kijiji hicho cha Lusungo Wilayani Kyela.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa kabla ya kutenda kosa hilo aliwavizia wazazi wa mtoto huyo ambao ni Semeni Ogada (28) naTumpale Sakwisya (20) wote wakazi wa kijiji cha lusungo wakiwa wamelala usingizi na kufungua mlango wa nyumba uliotengenezwa kwa matete kisha kumuiba mtoto na kukimbia nae.

Hata hivyo baba wa mtoto alishtuka na kupiga kelele za kuomba msaada hivyo majirani walijitokeza na kumkimbiza mtuhumiwa na kumkamata akiwa na mtoto huyo. Mtuhumiwa amejeruhiwa baada ya kushambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.

Mtuhumiwa aliokolewa na askari polisi waliofika eneo la tukio na amelazwa hospitali ya wilaya ya kyela akiwa chini ya ulinzi. Aidha mtoto amefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa wazazi akiwa salama.

MWISHO

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top