Askari akiongoza msafara Coastal Union |
Burudani |
Kocha Chipo akizungumza na Waandishi wa Habari. |
NA
MWANDISHI WETU,TANGA.
MKUU wa
wilaya ya Tanga,Halima Dendego leo ameongeza mapokezi ya timu ya Coastal Union
yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ndege jijini Tanga ambapo timu hiyo ilikuwa
ikitokea Visiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi kwa muda wa mwezi mzima.
Akizungumza
wakati wa mapokezi hayo DC Dendego amesema kuwa serikali ya wilaya hiyo
haitasita kuchukulia hatua watu wote wanaoleta migogoro na chokochoko ndani ya
klabu ya Coastal Union kwa sababu wasiposhughulikiwa wanaweza kupelekea
kuwagawa wanachama,wapenzi na mashabiki hivyo kudhoofisha maendeleo.
Wachezaji
hao walitua uwanja wa ndege Tanga wakitumia ndege mbili tofauti ambapo baada ya
hapo Mkuu huyo wa wilaya aliweza kuongoza msafara wa magari zaidi ya
50,pikipiki na baiskeli zisizokuwa na idadi zilizunguka maeneo mbalimbali
jijini Tanga huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kuilaki kila ilipokuwa
ikipita kwa kuimba nyimbo za kuisifu timu hiyo.
Baada
ya mzunguko huo ambao ulichukua takribani saa moja ndipo wachezaji wa timu hiyo
wakawasili kambini eneo la Raskazone Hotel Pembezoni mwa bahari ya hindi ilipo
kambi yao hivyo.
Dendego
amesema kuwa lazima wao kama serikali wahakikisha klabu zao mkoani hapa
zinakuwa na utulivu kila wakati kwa hiyo inapotokea inakwenda kunyume chake
basi wao watachukua hatua kali ili iweza kuwa fundisho kwa watu wengine ambao
wanaweza kufanya hivyo kipindi kingine.
Hata hivyo amesema kuwa lazima
wapenzi ,wanachama na mashabiki kuhakikisha wanakuwa na mshikamano wa thati ili
kuweza kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yake waliojiwekea kwenye msimu
mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
Kwa
upande wake,Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesema kuwa timu hiyo
ilifanya usajili mzuri msimu huu hivyo wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri
kwa kuanzia na mechi yao na Simba ambao haiwapi wasiwasi wa aina yoyote ile.
El
Siagi amesema kutokana na maandalizi timu hiyo walioifanya wakiwa visiwani
Pemba wana matumaini makubwa ya kuibuka na pointi tatu muhimu mbele ya Simba
mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu itakayochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Awali
akizungumza katika mapokezi hayo,aliyekuwa Mwenyekiti wa Coastal Union,Hemed
Aurora amewataka wapenzi ,wanachama kudumisha na kuendeleza mshikamano ili
kuiwezesha timu hiyo kuweza kufikia malengo yao ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu
msimu ujao.
“Umoja na mshikamano ndio siri
ya mafanikio yoyote yale hivyo nawasihi wapenzi ,mashabiki na wanachama muenzi
mshikamno kwa sababu ndio nuru ya mafanikio kwenu “Alisema Aurora.
Post a Comment