Mwigizaji Jacob Steven ‘JB’, alizungumza na gazeti la Mtanzania hivi karibuni, wakati wa kongamano la amani lililoandaliwa na maaskofu na masheikh wa Mkoa wa Mwanza.
JB ambaye alikuwa ameongozana na wasanii wengine kama Mzee Majuto na Mrisho Mpoto, alisema mchakato wa kuandaa filamu hiyo umeanza.
“Tumeguswa na mauaji ya walemavu wa ngozi, ambayo yamekuwa yakitokea kila mara kanda ya ziwa, tutatengeneza filamu ambayo kila mtu akipata nafasi ya kuitazama itafikisha ujumbe wa kuacha kufanya mauaji,” alisema JB.
Kwa upande wake, Mzee Majuto, alisema umefika wakati suala la mauaji ya watu wenye ulemavu yakamalizika na kukomeshwa kabisa.
Picha hapo juu zimetoka kwenye makala ya BBC.
Post a Comment