Makao makuu ya kanisa katoliki
duniani Vatican yanasema kuwa nguvu inaweza kutumiwa kusitisha
mashambulizi yanayoendeshwa na wanamgambo wa Islamic State dhidi ya
wakristo na makundi mengine madogo .
Askofu mkuu Silvano Tomasi
ambaye ni mwakilishi mkuu wa Vatican kwenye umoja wa mataifa mjini
Geneva ameyashutumu makundi ya jihad kwa kuendesha mauaji ya halaiki.
Akizungumza kupitia mtandao wa Vatican amesema kuwa hatua za kijeshi zitaanzishwa ikiwa suluhu ya kisiasa haitapatikana.
Lakini amesema kuwa muungano wowote dhidi ya Islamic State ni lazima ujumuishe nchi za kiislamu kutoka mashariki ya kati.
Post a Comment