Burudani |
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mbeya, Amani
Kajuna, akizungumza kwenye sherehe za kuwaga wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya
Sekondari ya Usongwe, iliyopo Mbeya Vijijini.
|
Na Mwandishi wetu,Mbeya
CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya, kimewataka wanafunzi
wa sekondari ambao wamekidhi vigezo vya kuchagua kiongozi, kutokubali kutumika
kama madaraja ya kuwavusha wanasiasa wabovu,wasiokuwa na sifa kwa jamii.
Kimesema, viongozi wabovu na wasio na mapenzi na nchi
yao, wamekuwa na tabia ya kuwashawishi vijana kufanya vurugu au kuipotosha
jamii kwa kuwapa fedha.
Kauli hiyo, imetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa
Vijana wa CCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna, kwenye sherehe za kuwaga wanafunzi
wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Usongwe, iliyopo Mbeya
Vijijini.
Alisema,vijana hao wanapaswa kuwa makini sana, katika
kipindi hiki cha uchaguzi, kwani kunawimbi kubwa la viongozi wabovu wameonyesha
nia ya kuingia madarakani.
Alisema,nchi imekuwa ikiwategemea wanafunzi kwa kutoa
elimu kwa jamii juu ya masuala mbalimbali kama vile, umuhimu wa kuchagua
kiongozi bila ya kupokea fedha, kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura
pamoja na kuipigia kura katiba mpya hivyo wao wakiruhusu kutumiwa kwa maslahi
ya wachache, taifa litakuwa limeingia
kwenye matatizo ya umasikini.
Aidha, aliwahasa vijana kujikita zaidi kwenye shughuli za
maendeleo kwa kubuni miradi mbalimbali kuliko kusubili siku za uchaguzi na
kugeuza kama sehemu ya dili ya kupata fedha.
Mwisho.
Post a Comment