Mkutano ukiendelea |
Picha ya Pamoja na Mgeni rasmi. |
Na
Moses Ng'wat,Morogoro.
Na
Moses Ng'wat,Morogoro.
SERIKALI imeliagiza Shirikisho la
Riadha la Tanzania (RT) kuhakikisha
kuwa inafanyia kazi vipaumbele vitano vitakavyoweza kulinasua kutoka katika
mkwamo na kurudisha hadhi ya mchezo huo hapa nchini na duniani kote.
Ushauri huo ulitolewa jana na Naibu Katibu wa
Wizara ya, Prof.Elisante ole Gabriel, wakati akifungua mkutano Mkuu maalumu wa
kupitisha katiba ya shirikisho hilo, uliofanyika jana katika hoteli ya Gronency,
Mjini hapa.
Prof.Ole Gabrieli aliyemwakilisha Naibu Waziri
wa Wizara hiyo, Juma Nkamia, alisema ili Shirikisho hilo liweze kufanikiwa
kurudisha ufanisi wake katika kusimamia mchezo huo, linapaswa kuweka mikakati
mahususi.
Aliitaja mikakati hiyo mahususi
itakayowezesha kulikwamua shirikisho hilo kuwa ni RT kuunda jopo la wabobevu
watakaokuwa na kazi ya kufikiria namna ya kuipeleka mbele riadha.
Vipaumbele vingine vilivyotolewa
kama changamoto kwa RT ni kuweka Mipango Mkakati, malengo ya ushindi(Medali),kutafuta
wafadhili wa kudumu, pamoja na kutanua mtandao wa kiuhusiano na mataifa mengine
duniani.
"Serikali itaweza kuwasaidia kila kitu,
lakini kamwe msidhani kuwa serikali itakuja kuwasaidia namna ya
kufikiria....hivyo ni jukumu la kila kiongozi wa riadha katika ngazi zote
kuhakikisha anatumia uwezo wake kuisaidia riadha badala ya kuishia kulalamika
tu" alisisitiza Prof. Ole Gabriel.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi
katika mkutano huo, Rais wa shirikisho la Riadha nchini, Anton Mtaka, ambaye
pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro, alisema mchezo huo umekuwa
ukikabiliwa na changamoto kutokana na kukosa rasilimali fedha.
"Changamoto
za Tanzania katika mchezo wa riadha ni sawa na nchi nyingine duniani, kwani
imekuwa ikipokea ruzuku ndogo ya dola 15,000 kutoka kwa shirikisho la mchezo
huo duniani IAAF ambazo ni sawa kiasi cha shilingi milioni 20 kwa mwaka".
Hata hivyo, aliishukuru serikali kwa
mchango wake wa kuthamini michezo, hususani riadha kwa kuendelea kutoa udhamini
wa kupeleka wachezaji nje ya nchi kwa Ajili ya mazoezi
ya.kujianxaa na michezo mbalimbali ya.kimataifa
Mwisho.
Post a Comment