Wanawak ewa ushirika wa KKKT Usharika wa Ruanda Block T wakisiliza neno katika siku maombi ya wanawake Duniani iliyofanyika katika kanisa hilo leo Machi 6, 2015 |
Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Ndugu Amani Kajuna akizungumza na wanawake wa KKKT usharika wa Ruanda Block T. Mwanjelwa katika siku ya Maombi ya wanawake Duniani yaliyofanyika kanisani hapo. |
Mchungaji wa ushirika wa K.K.K.T Ruanda Felister akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi |
Ibada ikiendelea |
Wanawake wa kikistro Mkoani Mbeya wametakiwa kuendelea kukemea vitendo
viovu vinavyo fanywa na vijana hususani watoto wa kike ambao wengi
wao wamejiingiza katika biashara ya ngono pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UVCCM) Mkoa wa Mbeya
Ndugu Amani Kajuna katika siku ya Maombezi ya wanawake Duniani yaliyofanyika
katika Kanisa la K.K.K.T ,Ushirika wa Ruanda Mwanjelwa jijini hapa.
Amesema vijana wengi
hususani watoto wa kike wemepoteza maisha na wengine kuharibikiwa kutokana na
kujiingiza katika vitendo viovu hasa kwa matumizi ya madawa ya kulevya pamoja
na biashara ya ngono.
Amesema wahusika wa biashara ya madawa ya kulevya kwa
sasa wamebadilisha mbinu ya kuingiza na kusafirisha madawa ya kulevya kwa
kuwatumia zaidi watoto wa kike ambao hata hivyo wamekuwa wakikamatwa katika
viwanja vya ndege.
Kajuna amesema pamoja na
kujingiza katika biashara hiyo pia yameibuka matukio mbalimbali yasiyopendeza
katika jamii ambayo yamekuwa yakimuhusisha moja kwa moja mtoto wa kike hali
ambayo inafanya kundi hilo kutafsirika vibaya na jamiii.
Kufuatia hali hiyo Mwnyekiti
huyo ametoa wito kwa vikundi mbalimbali vya akina mama wa kikistro mkoani hapa
kukakikisha wanasaidiana na serikali katika kukemea hali hiyo vinginevyo
serikali itapoteza nguvu kazi ya taifa.
Wakati huo huo Mwenyekiti
huyo amewataka akina mama na wanawake wote kwa ujumla mkoani humo kujitokeza
kwa wingi katika kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili
waweze kuipigia kura katiba iliyopendekezwa ili iweze kupitishwa.
Amesema katiba hiyo kwa sasa
ina mambo mengi muhimu ambayo yanalenga kumkomboa mwanamke katika Nyanja mbalimbali
za kimaendeleo pamoja na kimamuzi ndani ya familia kwa ujumla.
Awali wakisoma risala kwa
mgeni rasmi akimama hao wa K.K.K.T usharika wa Ruanda walimuomba mgeni rasmi
kuwa saidia mambo mbalimbali ikiwemo suala la kuwaongezea mtaji katika kikundi
chao ambacho kwa sasa wanajishughulisha na ufugaji wa kuku pamoja na ukodishaji
wa maturubai ambapo hata hivyo Kajuna aliahidi kutoa kiasi cha shilingi Mil.1
mwishoni mwa mwezi huu .
Mwisho.
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment