Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo wa
madereva baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa
mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
(NIT)
Kuhusu suala la Madereva kusoma, Serikali na Madereva wamekubaliana kukutana
mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia mbadala ya kutumika.
Miongoni mwa malalamiko ya madereva ilikuwa ni kukerwa na tochi za
barabarani, hivyo jeshi la Polisi wamekubali kuziondoa.
Pia serikali imeagiza Madereva wote wapewe mikataba ya ajira za uhakika na
waajiri wao na Trafiki wameagizwa kulifatilia hilo.
Mapema leo Maelfu ya abiria walikwa kwenye
vituo vya mabasi nchini kutokana na mgomo huo wa madereva wa mabasi.
|
Post a Comment