Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwenyekiti wa Uvccm Mbeya Aman Kajuna akivishwa skafu na vijana wa skauti katika mahafali ya sita ya shule ya sekondari ya usongwe Mbalizi Wilayani Mbeya April 28 mwaka huu.


Wahitimu wa kidato cha sita katika mahafali ya sita ya shule ya sekondari usongwe Mbalizi Mbeya wakifurahia katika mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa ushule hiyo April 28 mwaka huu.



wahitimu wa elimu ya kidato cha sita katika mahafali ya sita ya shule ya sekondari Usongwe Mbalizi wilaya ya Mbeya wakisoma Lisara kwa mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyofanyika shuleni hapo April 28.



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (Uvccm ) Ndugu Aman Kajuna akitoa vyeti kwa wahitimu wa elimu ya kidato cha sita katika mahafali ya sita ya shule ya sekondari ya Usongwe Wilaya ya Mbeya April 28 mwaka huu.

wanafunzi wa shule ya sekondari ya Usongwe Mbalizi wakiimba wimbo wa pamoja katika mahafali ya sita ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo April 28 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna akizungumza katika mhafali ya sita ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Usongwe Mbalizi wilaya ya Mbeya




Picha ya pamoja mgeni rasmi Ndugu Amani Kajuna mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya na wahitimu wa elimu ya kidato cha sita katika shule hiyo ya Usongwe Mbalizi April 28.






Na Mwandishi wetu,Mbeya

Wito umetolewa kwa Wazazi na walezi Mkoani Mbeya kuhakikisha wanatenga muda wao kwa kukaa na vijana wao katika kuwajengea maadili mema badala ya kuwa tupia jukumu hilo walimu pekee.



Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi(UVCCM), Mkoa wa Mbeya, Ndugu Aman Kajuna katika mahafali ya 6  kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Usongwe Mbalizi wilaya ya Mbeya.



Kajuna amesema wazazi wengi wanafikiri kumaliza kulipa ada bila kufuatilia maendeleo ya mtoto amekuwa ametimiza wajibu wake jambo ambalo sio sahihi kwani kuna baadhi ya watoto ni wadanganyifu hawafiki shule hivyo ni wajibu wa mzazi kufuatilia mwenendo wake.



Amesema malezi ya mtoto yanatakiwa kuanzia nyumbani ba Kuhusu changamoto zilizotolewa na Shule hiyo, Kajuna alisema kutokana na wingi wa wanafunzi ulivyo suala la usafiri wa shule linapaswa kupewa kipaumbele cha pekee ili aweze kulitatua hilo. 



Ameema endapo wazazi watashiriki kikamilifu katika malezi ya watoto kwa kufuatilia nyendo zao kama wanahudhuria masomo kikamilifu itasaidia kuongeza ufaulu kwa mwanafunzi pale atakaoona anafuatiliwa kwa ukaribu kila kona



Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Ndugu Benedict Mahenge ametoa sababu mbalimbali zinazofanya wanafunzi washindwe kufanya vyema katika masomo yao.





Mahenge alisema shule hiyo haina ufaulu mzuri kwa wanafunzi wake hali inayotokana na wazazi kuwaachia jukumu la kuwalea wanafunzi walimu pekee wakisahau kuwa suala la malezi ya watoto linategemea pande zote mbili.





 Amesema changamoto kubwa ni  wazazi kushindwa kuwa karibu na watoto wao hali hiyo imesababisha kati ya wanafunzi 80 waliokuwa wamechaguliwa kujiunga kidato cha tano 2013, 57 pekee wamefanikiwa kuhitimu kidato cha sita mwaka huu huku 23 hawajulikani walikoishia.



Amesema changamoto nyingine ni  upungufu wa walimu wa hesabu, upungufu wa vitabu, majengo muhimu kama bwalo la chakula ambapo wanafunzi hulazimika kulia mabwenini jambo ambalo ni hatari.



Aidha kutokana na changamoto hizo Mgeni rasmi katika mahafali hayo Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Ndugu Amani Kajuna alisema itabidi akutane na Mkuu wa Shule ili waangalie uwezekano wa kupata gari litakalosaidia kulahisisha na kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi pindi dharula kama kuugua linapojitokeza.



Mwisho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top