Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baadhi ya vijana wakiwa katika mafunzo ya namna ya ufyatuaji wa matofali na ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika eneo la ofisi za Vicoba Mbeya Nanenane ambapo mradi huo kwa asilimia kubwa umefadhiriwa na shirika la nyumba la Taifa NHC.



Tofali za mfano zinazofyatuliwa katika mshine za kisasa zilizo tolewa na shirika la nyumba la kwa taifa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kujenga nyumba bora za kisasa zenye gharama nafuu kwa matofali ya kufungamana .




Maabara kwa ajili ya kupimia aina ya udongo utakao tumika katika ufyatuliaji wa tofali hizo.

Mkurugenzi mtendaji wa ofisi ya Vicoba Mkoa wa Mbeya Ndugu Bosco Mdelwa akionyesha mfano wa udongo ambao umefanyiwa vipimo tayari kwa ajili ya ujenzi na ufyatuaji wa tofali za kufungamana mradi ambao kwa asilimia kubwa umetolewa na shirika la nyumba la Taifa.





Mtaalamu wa masuala ya ujenzi katika ofisi ya vicoba Mbeya Ndugu Elias Mwahambi akitoa maelekezo kwa mmoja wa waandishi wa habari aliyetembelea ofisi hizo kwa lengo la kujifunza na kufahamu jinsi ofisi za vicoba zilivyo weza kusaidia vijana katika utekekelezaji wa mradi huo.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0759 406 070

Post a Comment

 
Top