Na Herman Kihwili
Kocha wa timu ya mpira wa magongo Varentina Quaranta amesema anaamini timu za Tanzania zitafanya vizuri katika michezo iliyobaki katika mashindano ya kuwania kufuzu michuano ya Olympic ya mwaka 2016 ambayo yatafanyika mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil, licha ya kufanya vibaya katika michezo yao ya awali.
Varentina Quaranta ambaye Yuko nchini Afrika Kusini na Timu za Tanzania za Wanawake na wanaume,zinazoshiriki mashindano hayo,amesema kufanya vibaya kwa timu za Tanzania kunatokana na kiwango kidogo kwa timu zetu.
Varentina
Quaranta amewapongeza wachezaji wa Tanzania kwa kupambana katika
mashindano hayo,lakini kwanza akianza kwa kuelezea matokeo ya michezo
kwa timu za Tanzania.
Post a Comment