"Wakati wa kupiga picha, waliiona treni ikija wakasongea kando.
Lakini treni nyingine ilitokezea upande wa pili na walikwama katikati.
Waligongwa na mojawapo ya treni hizo," Indian Express ilimnukuu afisa wa
polisi.
Afisa mmoja wa polisi wa reli ameongeza kuwa vijana hao walimkodisha mpigaji picha mtaalamu kwa kazi hiyo.
"Tumeipata
kamera kutoka kwa vijana iliotumika. Mlikuwa na picha na video, Video
inakaguliwa, wakati picha hizo zinathibitisha kuwa walikuwa wanaruka
kutoka reli moja hadi nyengine," Naibu kamishna wa polisi Parwaiz Ahmed
ameiambia Hindustan Times.
Mwaka jana wanafunzi wawili walizama
walipokuwa wanapiga selfi katika mto uliofurika katika eneo la jimbo la
kaskazini la Uttar Pradesh.
Na polisi mjini Mumbai imetaja maeneo
15 ambapo 'ni hatari' kupiga Selfie baada ya msichana wa miaka 18
kuzama baharini wakati akijipiga selfie.
Post a Comment