Mwenyekiti
wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya
wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam ametoa msaada wa pampu ya
maji na mifuko 10 ya saruji vyenye thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa
ajili ya kumaliza tatizo la maji katika kitongoji cha Mwamapalala kata
ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga.
Mukadam
amekabidhi msaada huo wa pampu ya maji na mifuko ya 10 ya saruji kwa
diwani wa kata ya Chibe John Kisandu leo Ijumaa Novemba 17,2017 kwa
ajili ya mradi wa maji katika mtaa wa Mwamapalala katika kata hiyo
ambayo inakabiliwa na kukosekana kwa huduma ya maji.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo,Mukadam alisema hivi karibuni
alitembelea kata ya Chibe,ndipo diwani wa kata hiyo akaomba msaada wa
kutafutiwa pampu ya maji baada ya wananchi kujitolea kuchimba kisima
kirefu.
“Kutokana
na ombi hilo,nimetafuta wafadhili na kupata msaada huu kutoka kwa
Farana Hirji aliyenipatia fedha kwa niaba ya Roshan Chatur nikanunua
pampu hii na saruji hii itakayotumika kukamilisha ujenzi wa
kisima”,alieleza Gulam.
“Kupitia
msaada huu wananchi wa Chibe watapata huduma ya maji safi na salama
kwani mhandisi wa maji wa manispaa amefika katika kisima hicho na
kutuhakikishia kuwa maji hayo ni salama kwa matumizi ya
binadamu”,alisema Mukadam.
Hata
hivyo alisema aliwataka wadau kuendelea kushirikiana na serikali katika
kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kama vile
maji,afya na elimu. Naye
Kaimu katibu mkuu ALAT,Abdallah Ngodu ambaye yupo katika ziara
kutembelea halmashauri mbalimbali nchini,alimpongeza Gulam kwa jitihada
anazochukua katika kumaliza kero za wananchi.
“Lengo
la ALAT ni kuhakikisha tunatatua kero za jamii ambazo nyingi zipo
katika sekta ya maji,afya na elimu,hivyo kwa kushirikiana na serikali
tutaendelea kutatua changamoto hizi”,alisema Ngodu.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Rajabu Masanche alikiri kuwepo
kwa changamoto za maji katika manispaa hiyo hivyo kuwaomba wadau
kujitokeza kusaidia huku akiwataka wananchi kutunza miundombinu ya
maji.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Chibe,John Kisandu alimshukuru Mukadam kwa
kumpatia msaada huo ambao utakuwa msaada kwa wananchi hao ambao
wanakabiliwa na tatizo la maji.
“Kata
ya Chibe ina wakazi zaidi ya 3,000 na kuna mitaa minne ambayo ni
Busambilo,Chibe,Mwalugoye na Mwamapalala,mitaa yote ina shida ya
maji,wananchi wa Mwamapalala walijitolea kuchimba kisima nikamuomba
mheshimiwa Gulam atupatie msaada wa pampu na leo ametupatia,tunamshukuru
sana”,alieleza Kisandu.
Zoezi
la kushusha pampu ya maji kwenye gari likiendelea wakati Mwenyekiti wa
Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikabidhi pampu ya maji na
mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kisima kirefu cha maji katika
kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga- Picha zote na Kadama Malunde -
Malunde1 blog
Kaimu
Mhandisi wa maji manispaa ya Shinyanga Nkinda Seni (wa nne kushoto)
akishusha mabomba ya pampu ya maji.Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya
wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa
kukabidhi pampu ya maji na mifuko ya saruji kwa diwani wa kata ya Chibe
John Kisandu kwa ajili ya ujenzi wa kisima kirefu katika mtaa wa
Mwamapalala. Kushoto ni pampu ya maji na mifuko ya saruji.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya
wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akishikana mkono na
diwani wa kata ya Chibe John Kisandu wakati wa akikabidhi pampu ya maji
na mifuko ya saruji.Wa kwanza kulia ni Kaimu katibu mkuu ALAT,Abdallah
Ngodu na Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Rajabu Masanche
wakishuhudia zoezi la makabidhiano.
Wa
kwanza kushoto ni Kaimu Mhandisi wa maji manispaa ya Shinyanga Nkinda
Seni na Katibu tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi wakishuhudia
tukio la makabidhi
Kaimu
katibu mkuu ALAT,Abdallah Ngodu akimpongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya
serikali za mitaa nchini Tanzania (ALAT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kushoto) kwa kutoa msaada wa pampu ya
maji katika kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga.
Kaimu katibu mkuu ALAT,Abdallah Ngodu akishikana mkono na diwani wa kata ya Chibe,John Kisandu.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Post a Comment