Makamu Rais wa TCCIA Tanzania Ndugu
Julius Kaijage katikakati akizungumza juu maandalizi ya safari hi
|
Home
»
»Unlabelled
» ZAIDI YA WAFANYABIASHARA 100 KUTOKA MIKOA YA MBEYA,IRINGA,NJOMBE KUHUDHURIA MAONESHO NCHINI AFRIKA KUSINI
Mkurugenzi
wa Blue Bird Burue De Change ya jijiji Mbeya Ndugu Janko Ndigo wa
kwanza kushoto akizungumzia juu ya ushiriki wa kampuni ya yake juu ya
ushiriki wa maonesho hayo - See more at:
http://jamiimoja.blogspot.com/2015/02/wafanyabiashara-zaidi-100-kutoka-mikoa.html#sthash.nKhTlXrj.dpuf
Mkurugenzi
wa Blue Bird Bureau de Change ya jijiji Mbeya Ndugu Jankey Ndingo wa kwanza
kushoto akizungumzia juu ya ushiriki wa kampuni ya yake juu ya ushiriki wa
maonesho hayo
Na Mwandishi wetu,Mbeya
ZAIDI ya wafanyabiashara 100 wadogo na wakubwa nchini, wanatarajia
kwenda kuzulu Afrika ya kusini ikiwa na kuhudhuria maonesho ya biashara
yajulikanayo kama Esther Land Show.
Maonesho hayo ya kitaifa yanatarajia kufanyika, April mwaka huu,
katika mji wa Johnsburg Afrika ya kusini kwa udhamini wa kampuni ya
Blue Bird Buleau De Change iliyopo Jijini Mbeya.
Akizungumza jijini mbeya, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Jankey
Ndingo, alisema ziara hiyo imelenga kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania
na nchi ya Afrika ya kusini katika kujengeana uwezo ikiwa na kutangaza fursa
zilizomo kwenye maeneo yao.
“Mji wa Johnsburg umekuwa ukiendesha maonesho ya biashara kila
mwaka katika Sikukuu ya Pasaka, hivyo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa
wakihudhuria maonesho haya lakini kwa mwaka huu tunataka kuwashirikisha wafanyabiashara
wadogo ili nao wafike na kunufaika na fursa hiyo,”alisema.
Alisema, maonesho hayo yamejikita zaidi katika masuala ya matumizi
ya mitambo mbalimbali kama vile mitambo ya kilimo,vifungashio pamoja na ile
inayozalisha bidhaa zikiwa na kiwango cha ubora unaoendana na soko la
kimataifa.
Alisema, Afrika kusini kumekuwa na soko kubwa la bidhaa za
kitamudi na zao la tangawizi zinazozalishwa Tanzania hivyo ni vema
wafanyabiashara wakatumia fursa hiyo kwenda kutafuta masoko na kuanza
kusafirisha bidhaa hizo.
“kinachotakiwa kufanywa na wazalishaji ni kuhakikisha bidhaa zote
zinakidhi kiwango cha ubora wa kimataifa,”alisema.
Aidha, alisema kuwa ziara hiyo inashirikisha wafanyabiashara wote
wanaonesha nia ya kutaka kujifunza na kubadilika ili kuondoka na hali ya
umaskini na kwamba safari hiyo itaanzia Mjini Mbeya kwa usafiri wa basi
kupitia njia ya Zambia na kwa gharama nafuu.
Hata hivyo, alisema kuwa safari hiyo itakuwa ni ya kitalii zaidi
kwani wafanyabiashara watapata fursa ya kutembelea maporomoko ya mto Zambezi
yajulikanayo kama Victoria yaliyopo nchini Zambia na kwamba ziara hiyo itakuwa
ya siku 13.
Mwisho.
Recent Posts
- MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WAHALIBIFU WA VYANZO VYA MAJI07 Nov 20181
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Meryprisca Mahundi (katikati) akimkisikiliza kwa makin...Read more ?
- 25 Oct 20180
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila (wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa ...Read more ?
- 25 Oct 20180
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila (wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa ...Read more ?
- MHAGAMA AAGIZA NEEC KUFANYA TATHIMINI YA UHALISIA WA WANUFAIKA WA MIKOPO INAYOTOLEWA NA TAASISI ZA KIFEDHA20 Oct 20180
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenis...Read more ?
- MK17 Oct 20180
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhandisi Meryprisca Mahundi (kushoto) akisikiliza meelezo kutoka kwa mmoj...Read more ?
- BABA AMUUA MTOTO WAKE KWA SUMU MBEYA31 Aug 20180
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.