Naibu waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye pili kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa mafundi ya karakana ya Reli ya Tazara iliyopo katika kituo cha Iyunga Jijini Mbeya |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditiye amewaagiza askari polisi kitengo cha reli kuwakamata watu
wanaotuhumiwa kupiga mawe treni pindi zinapopita kwenye maeneo yao na
kuhasababisha uharibifu ambao huigharimu serikali pesa nyingi katika
matengenezo vingine watawajibishwa wao
Hayo
yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi. Atashasta Nditiye,
alipotembelea Kalakana ya Tazara iliyopo Jijini Mbeya.
Amesema
wapo baadhi ya watanzania wamekuwa wakiendelea
na vitendo vya kuhujumu treni hivyo lazima wachukuliwe hatua kali ili kukomesha
vitendo hivyo kwa kuhakikisha zinatolewa adhabu kali kwa watako bainika kufanya
vitendo hivyo.
Waziri Nditiye amewataka madereva wa treni kusimamisha treni endapo
itatokea kuna baadhiya watu wamefanya tukio la kupiga mawe treni mara iwapo
safarini ili wahusika wakamatwe na
kuhojiwa ili watoe sababu za kufanya kitendo hicho sanjali na kuchukuliwa hatua
mara mora .
Wakati
huo naibu Waziri , amewahakikishia wanyabiashara na
wachuuzi kuwa hatua ya uimarishaji wa usafiri na usafirishaji kupitia Reli
nchini,uko pazuri na tayari muda wa kuondoa mizigo mizito inayotumia malori
umefika
Amesema,katika
kuimarisha usafiri huo, zaidi ya shilingi bilioni 10 zimetolewa na serikali
kuboresha vichwa vya magari moshi na kalakana mbalimbali nchini.
Amesema,
serikali haitegemei kuona malori ya kiendelea kusafirisha mizigo mizito ambapo
wakati mwingine yamekuwa chanzo cha kuharibu miundombinu ya barabara pamoja na
kuua soko la Tazara.
“Barabara
hizi zimejengwa kwa gharama kubwa sana, tunategemea mizigo hiyo kuanza
kusafirishwa kwa kutumia njia ya reli na kwamba ni jukumu la wafanyakazi kuanza
kuwashawishi wateja wao wazamani na wapya ili wafanye kazi na
Tazara,”amesema.
Hata
hivyo amesema ,serikali haiwezi kuendelea kuwalipia mishahara lazima itafika
pahala ambapo itasitisha na kuiacha Tazara iendelee na majuku yake kwa
kujiendesha yenyewe, hivyo wanapaswa kujipanga kwa kuwa wabunifu.
mwisho.
Post a Comment