Machinjio ya Ng'ombe eneo la Veta mbeya ambayo imefungwa na Halmashauri ya jiji la Mbeya kwa madai kuwa miundombinu yake kutokuwa salama kiafya ambapo kwasasa imefika mwezi toka kufungwa kwakwe. |
Hatua ya Halmashauri ya jiji la Mbeya kuamua kuifunga machinjio Ng'ombe iliyopo eneo la Veta jijini hapa kwa madai kuwa
baadhi ya miundo mbinu yake kuto kuwa
mizuri hali hiyo imeathiri kwa kiasi
kikubwa biashara ya nyama ndani ya jiji hilo.
Toka kufungwa machinjio inadaiwa kufika
mwezi sasa hali ambayo imechangia kwa kiwango kikubwa kuadimika nyama kwa pamoja na kupanda kwa bei ambapo kwa sasa kilo
moja huuzwa kwa shilingi 6000 hadi 7000 kutoka shilingi 4500.
Imeshuhudiwa baadhi ya wafanya biashara
wanaomiliki mabucha kuanza kuagizia bidhaa hiyo kutoka Tukuyu Wilaya ya Rungwe Mkoani hapa.
Baadhi ya wafanyabiasahara hao wakizungumza
na blog hii wamedai kuwa wanalazimika kupandisha bei hiyo kutokana na
kuifuata mbali nyama hiyo hivyo sauala
la kupanda kwa bei kunatokana na kufidishia gharama za usafirishaji.
Wamesema biashara hiyo imekuwa ngumu
kutokana na kupanda kwa bei yenyewe hivyo wengi wanashindwa kuhimili bei hiyo.
Wamesema wao hawapingani na uongozi wa jiji
kuchukua hautua hiyo lakini kinacho washangaza nikuona mapaka sasa hakuna maboresho yoyote
yanayofanyika katika machinjio hayo.
Akizungumzia hali hiyo Mkurugenzi wa jiji
la Mbeya Mussa Zungiza amesema halmasahuri ya jiji iliamua kuchukua hatua hiyo
kutokana na mazingira ya machinjio hayo kutokuwa katika hali ya usalama kiafya.
Amesema mara nyingi wafanyabiashara
wamekuwa wakilalamika mara baada ya halimashauri kuchukua hatua lakini wao
kufanya marekebisho mapema kabla ya kutokea kwa mapungufu hayo inakuwa ngumu
hasa kutokana na wao kuwa kimaslahi zaidi.
Amesema kwa sasa machinjio inayotumika ni
ile ya Uyole na Mbalizi wakati taratibu zingine zikiendelele ili kurudisha
machinjio hayo katika hali ya ambapo tayari wamekwisha tangaza zabuni .
Aidha amesema kuwa kitakachofanyika kwa
sasa ni kuhakikisha watakao chukua
zabuni hiyo wanafanya maboresho hayo kabla ya sikukukuu ya Kristimas ili
kuondoa adha hiyo kwa wananchi .
Mwisho.
Post a Comment